Discover millions of ebooks, audiobooks, and so much more with a free trial

Only $11.99/month after trial. Cancel anytime.

Wale Wenye Kiburi
Wale Wenye Kiburi
Wale Wenye Kiburi
Ebook140 pages3 hours

Wale Wenye Kiburi

Rating: 5 out of 5 stars

5/5

()

Read preview

About this ebook

Unyenyekevu ni sifa muhimu ya kiroho. Watu wachache walijaribu kuandika juu ya hii sifa ya kiroho ambayo si dhahiri ila muhimu. Katika juzuu hii mpya ya kusisimua, Dag Heward-Mills alifunua aina nyingi ya kiburi zinazotatiza. Hiki Kitabu kizuri, kilichoandikwa na mwenza Mkristo anayepambana pia, kitakubariki na kukutia moyo kujenga unyenyekevu wa kitoto wa Yesu Kristo.

LanguageKiswahili
Release dateApr 7, 2018
ISBN9781641345545
Wale Wenye Kiburi
Author

Dag Heward-Mills

Bishop Dag Heward-Mills is a medical doctor by profession and the founder of the United Denominations Originating from the Lighthouse Group of Churches (UD-OLGC). The UD-OLGC comprises over three thousand churches pastored by seasoned ministers, groomed and trained in-house. Bishop Dag Heward-Mills oversees this charismatic group of denominations, which operates in over 90 different countries in Africa, Asia, Europe, the Caribbean, Australia, and North and South America. With a ministry spanning over thirty years, Dag Heward-Mills has authored several books with bestsellers including ‘The Art of Leadership’, ‘Loyalty and Disloyalty’, and ‘The Mega Church’. He is considered to be the largest publishing author in Africa, having had his books translated into over 52 languages with more than 40 million copies in print.

Related to Wale Wenye Kiburi

Related ebooks

Reviews for Wale Wenye Kiburi

Rating: 5 out of 5 stars
5/5

1 rating0 reviews

What did you think?

Tap to rate

Review must be at least 10 words

    Book preview

    Wale Wenye Kiburi - Dag Heward-Mills

    Sura ya 1

    Jinyenyekeze

    Jidhilini mbele za Bwana, naye atawakuza.

    Yakobo 4:10

    Watu hufafanua kiburi katika namna nyingi tofauti. Watu wanaweza kusema una kiburi kwa sababu wewe ni mtu mkimya. Watu wanaweza kusema una kiburi kwa sababu wewe ni mrefu na unajiamini. Watu wanaweza kusema una kiburi kwa sababu unaendesha gari zuri linalong’aa lenye kiyoyozi.

    Kwa hiyo kiburi ni nini hasa? Je, inajalisha kama wewe ni mnyenyekevu au mwenye kiburi?

    Hakika inajalisha! Lazima tunyenyekee mbele ya Mungu. Lazima tuishi kwa namna ambayo Mungu anafikiria ni ya unyenyekevu..

    Agizo lipo wazi! Jidhihili mbele za Bwana na sio mbele ya watu. Haina maana kuonyesha aina ya unyenyekevu ambayo Mungu haikubali. Unyenyekevu ni maadili inayofafanuliwa na kuelezewa na Mungu mwenyewe. Wanadamu huelezea unyenyekevu kwa namna nyingi tofauti lakini ufafanuzi wa Mungu wa unyenyekevu ndo muhimu kwetu sisi.

    Unyenyekevu ni muhimu kana kwamba inapaswa mistari kutafutwa kwa marefu na mapana mpaka pale tutakapojua kwa uhakika ni nini. Maonyo kuhusu kiburi yanaogopesha sana kupuuzia.

    Katika sura hii ya kwanza, nataka tuangalie sababu kwa nini tunatakiwa kunyenyekea mbele za Bwana.

    Sababu saba kwa nini unatakiwa kujinyenyekeza.

    1. Jinyenyekeze kwa sababu Mungu huwapinga watu wenye kiburi.

    Lakini hutujalia sisi neema iliyozidi; kwa hiyo husema, MUNGU HUWAPINGA WAJIKUZAO, bali huwapa neema wanyenyekevu.

    Yakobo 4:6

    Kiburi ni kinyume sana na Mungu kana kwamba ametangaza vita kwa wote ambao wana kiburi. Unapokuwa na kiburi, Mungu atakuwa adui yako na atakupinga katika yote ufanyayo.

    Watu wanaokuwa na kiburi mara nyingi hawatambui kwamba Mungu ameanza kuwapinga. Wakati mwingine, wakristo humkemea shetani kwa sababu wanafikiri shetani ndio anayepigana nao. Lakini inapowahusu wakristo wenye kiburi, shetani anaweza kwenda likizo. Mungu mwenyewe huwapinga wenye kiburi.

    Unaweza hata ukajikuta unamkemea Mungu kwa sababu anakupinga wewe na kiburi chako. Sitapenda kumkemea Mungu, wewe je? Sitapenda Mungu awe adui yangu. Je ungependa Mungu awe adui yako? Mungu pekee ndiye anakupenda jinsi ulivyo. Kama akiwa adui yako pia, je nini kimebaki kwako?

    2. Jinyenyekeze kwa sababu Mungu huwapa neema watu wanyenyekevu.

    Lakini hutujalia sisi neema iliyozidi; kwa hiyo husema, MUNGU huwapinga wajikuzao, bali HUWAPA NEEMA WANYENYEKEVU.

    Yakobo 4:6

    Cha kushangaza, Mungu huwapa msaada usiostahiliwa watu wenye unyenyekevu. Neema ni msaada usiostahiliwa na kibali. Unapojishusha, Mungu anaitikia kwa kukutumia neema. Ni nzuri kiasi gani kupokea msaada usiostahiliwa unapochukua ile njia ya unyenyekevu! Pengine hamna sababu nzuri zaidi ya kujinyenyekeza kuliko hii. Fikiria kuhusu msaada wote usiostahiliwa ambao unaweza kupata maishani mwako na kwenye huduma yako kama ungejinyenyekeza.

    Unataka Mungu akupe msaada usiostahiliwa kanisani kwako? Je unataka Mungu akupe msaada usiostahiliwa kwenye huduma yako ya uchungaji? Basi jinyenyekeze! Unataka Mungu akupe msaada usiostahiliwa katika huduma yako ya uinjilisti? Basi jinyenyekeze!

    Je unataka Mungu akupe msaada usiostahiliwa katika mambo yako ya kifedhao? Basi jinyenyekeze! Je unataka Mungu akusaidie katika maisha yako ya kimaadili? Basi jinyenyekeze! Je unataka Mungu akupe msaada mwingi ili uwe mtakatifu? Basi jinyenyekeze! Karibia kila tukio la kiroho linasaidiwa na unyenyekevu.

    Pale unapojinyenyekeza unapewa msaada wa kimungu. Jaribu uone. Kuwa mnyenyekevu! Kuwa kama mtoto na mtumishi na uone kama mabadiliko hayatatokea katika maisha yako.

    Je kuhusu ndoa yako? Je unataka Mungu akusaidie katika mahusiano yako magumu? Kujinyenyekeza ni funguo ya kupokea msaada usiostahiliwa.

    3. Jinyenyekeze kwa sababu kupitia hivyo utainuliwa kwenye hatua inayofuata katika maisha.

    Jidhilini mbele za Bwana, NAYE ATAWAKUZA.

    Yakobo 4:10

    Sababu muhimu nyingine ya wewe kuwa mnyenyekevu ni kwa ajili ya kupandishwa cheo. Ni nani hataki kuinuliwa na kupandishwa cheo. Kuinuliwa na Bwana na kupandishwa na Bwana ni zawadi unazozipokea kwa kuwa mnyenyekevu. Angalia mstari vizuri. Unapoenda chini, Mungu atakuinua.

    Je hutafuti kuongezeka na kupandishwa cheo? Basi jinyenyekeze na uwe mtumishi! Jinyenyekeze na uwe mtoto ambaye anaweza kufunzwa na kuelekezwa.

    Utajikuta unapanda kutoka hatua ya sasa katika kiwango ambacho hujawahi kuota.

    Basi nyenyekeeni chini ya mkono wa Mungu ulio hodari, ili AWAKWEZE KWA WAKATI WAKE;

    1 Petro 5:6

    Fikiria. Inamaanisha nini kuinuliwa? Kuinuliwa ni kuinuliwa kiutukufu katika uzuri na ubora unaong’aa. Je sio hicho unachotaka? Unyenyekevu ndio funguo ya kuingia katika kiwango hiki.

    4. Jinyenyekeze ili kwamba ufunikwe na ulindwe.

    Vivyo hivyo ninyi vijana, watiini wazee. Naam, ninyi nyote JIFUNGENI UNYENYEKEVU, mpate kuhudumiana; kwa sababu Mungu huwapinga wenye kiburi, lakini huwapa wanyenyekevu neema.

    1 Petro 5:5

    Unyenyekevu ni kifuniko cha kiroho. Unyenyekevu sio mtazamo. Unyenyekevu sio namna ya kuishi kimaskini na kirahisi. Unyenyekevu sio namna ya kuonekana mwenye aibu na aliyeshindwa. Unyenyekevu hakika ni vazi la kiroho ambalo hukufunika. Humlinda mkristo kutokana na maovu mengi yasiyoonekana na maafa ya kiroho. Vaa unyenyekevu na utafunikwa, utakombolewa na kulindwa kutokana na maovu mengi ya maisha haya.

    5. Jinyenyekeze kwa sababu kiburi chako ni ishara ya maangamizi yako ya hivi karibuni, kuanguka kwako na aibu yako.

    KIBURI CHA MTU KITAMSHUSHA; Bali mwenye roho ya unyenyekevu ataheshimiwa.

    Mithali 29:23

    KIBURI HUTANGULIA UANGAMIVU; Na roho yenye kutakabari hutangulia maanguko.

    Mithali 16:18

    KIJAPO KIBURI NDIPO IJAPO AIBU; Bali hekima hukaa na wanyenyekevu.

    Mithali 11:2

    Kiburi ni ishara! Huashiria kuanguka kunakokuja, janga linalokuja na uovu unaokuja. Kujinyenyekeza kutaondoa hatari zinazokuja katika maisha yako na huduma yako. Shetani amevutiwa sana na kujiinua kwako na matamko yako ya kupitiliza. Ndiyo mlango uliowazi kwake yeye shetani.

    Kiburi ni ishara ya kiroho ambayo hukusanya mapepo ya aibu, uharibifu na kushindwa. Kiburi chako ni kama tarumbeta ambayo inatoa wito wa uhakika kwa roho mbaya. Unapokuwa na kiburi, malaika hawaruhusuwi kukusaidia. Unapokuwa na kiburi, mapepo wanakusanywa kukuharibu. Wewe kwa kweli unakuwa wazi kupatikana sana na mapepo kwa sababu nguo zako za kiroho na mavazi ya kujifunika yametolewa.

    6. Jinyenyekeze mbele ya Bwana kwa sababu kiburi kimsingi ni cha shetani na mapepo.

    Je! Waweza wewe kumvua mamba kwa ndoana? Au, kuufunga ulimi wake kwa kamba?, Yeye hutazama kila kitu kilicho juu; NI MFALME JUU YA WOTE WENYE KIBURI.

    Ayubu 41:1, 34

    Watu wote wenye kiburi wana mfalme na huyo mfalme ni shetani. Shetani ni mfalme wa watoto wote wenye kiburi. Lazima uamue kunyenyekea ili shetani asiwe mfalme na kiongozi wako. Kadiri unapokuwa na kiburi, utaishi na kutembea chini ya mwongozo wa shetani mwenyewe.

    Kimsingi kiburi ni mapepo na kishetani. Shetani alianguka kutoka mbinguni kupitia ufidhuli, majisifu na kiburi. Katika kiburi alijiinua dhidi ya Mungu! Shetani alijiinua dhidi ya kiti cha enzi chake Mungu na kutishia kupaa na kuchukua nafasi ya Mungu kwenye kiti chake cha enzi. Huu ndio ulikuwa udhihirishaji wa ujeuri wa hali ya juu ambao haujawahi kutokea.

    Lakini Mungu alimtupa shetani kutoka mbinguni na akamwonyesha kwamba hakuwa kitu chochote ila tawi lililoasi, na kujikuza bila sababu yoyote. Huku kujikuza na kujiinua ndio kunakoathiri jamii mzima ya mwanadamu. Wanadamu hujiona wakubwa na wakuu bila kuwa na sababu yoyote nzuri. Leo, sehemu kubwa ya jamii ya wanadamu kwa ujinga husema hamna Mungu.

    Kwa bahati mbaya, sisi watumishi wa injili pia tunajikuza tunapofanikisha malengo madogo madogo kwenye huduma. Kiburi sana huwa hakina msingi. Mara nyingi, Kiburi ni kitu kisicho na sababu (isiyojulikana). Watumishi wa injili wanajikuza na kuwavamia baba zao wa kiroho waliowalea. Wachungaji wasaidizi hujikuza na kujaribu kupanda kwenye kiti cha kiongozi. Wanajeshi huinuka na kujaribu kuwaondoa viongozi mataifa waliochaguliwa kiuhalali. Hivi vitu hutokea kwa sababu watu hujikuza na kujiona wakubwa kuliko walivyo.

    Maneno ‘kiburi’ na ’shetani’ yanafanana. Shetani ni roho! Lakini kiburi ni tabia na matamshi zinazosababishwa na uwepo wa shetani!

    Wakati wowote ambao utaona kiburi ndani ya mtu binafsi, unagundua uwapo wa roho mbaya- shetani! Shetani ndiye mwanzilishi wa kiburi. Hiyo ndiyo maana Mungu anachukia kiburi na anampinga mtu yeyote ambaye atamhisi ana kiburi!

    7. Jinyenyekeze mbele ya Bwana kwa sababu kiburi chako kitakufanya wewe uwe chukizo kwa Mungu.

    Kila mwenye moyo wa kiburi NI CHUKIZO KWA BWANA; Hakika, hatakosa adhabu.

    Mithali 16:5

    Mungu hampingi tu mwenye kiburi, lakini wenye kiburi ni chukizo kwake.

    Hili andiko linamaanisha ya kwamba Mungu anakasirishwa na watu wenye kiburi. Hawapendi wakaidi. Sio kitu kizuri kwa Mungu kukuchukia na kutokupenda. Nakushauri ugeuke kutoka kila kitu kinachohusiana na kiburi ili Mungu asije akajazwa na mageuzi na machukizo anapokuwazia wewe.

    Sura ya 2

    Jinsi ya Kuwa Mnyenyekevu Kama Mtoto

    Akasema, Amin, nawaambia, Msipoongoka na KUWA KAMA VITOTO,

    Mathayo 18:3

    AWE KAMA ALIYE MDOGO;…

    Luka 22:26

    Nini kanuni ya unyenyekevu? Tunawezaje kupata maadili haya ya kiroho isiyojulikana? Kwa sababu kiburi ni uovu usio dhahiri na usioelezeka, hujibadilisha kirahisi na kutujia sisi kwa namna nyingi mbalimbali. Sio jambo la kustaajabisha kwamba watu wengi wanaokiri kuwa wanyenyekevu kwa ukweli wana kiburi. Pia sio kitu cha ajabu kwamba mambo mengi yanayoitwa ya unyenyekevu kwa uhakika sio ya unyenyekevu. Kwa mfano, watu wanaozungumza kwa lafudhi fulani hudhaniwa kuwa na kiburi. Watu matajiri, watu wanaojionyesha na watu

    Enjoying the preview?
    Page 1 of 1