Discover millions of ebooks, audiobooks, and so much more with a free trial

Only $11.99/month after trial. Cancel anytime.

Jinsi Unavyoweza Kutimiza Huduma Yako
Jinsi Unavyoweza Kutimiza Huduma Yako
Jinsi Unavyoweza Kutimiza Huduma Yako
Ebook130 pages52 minutes

Jinsi Unavyoweza Kutimiza Huduma Yako

Rating: 5 out of 5 stars

5/5

()

Read preview

About this ebook

Dag Heward-Mills ni mwandishi wa vitabu vingi, ikiwemo kitabu kinachouzwa sana "Uaminifu na Ukosefu wa Uaminifu". Yeye ni mwanzilishi wa dhehebu lenye makanisa zaidi ya elfu moja linaloitwa "The Lighthouse Chapel International". (Kanisa la Kimataifa la Lighthouse). Dag Heward-Mills, mwinjilisti wa kimataifa huhudumu katika Mkutano wa Injili wa Kimataifa na Yesu Mponyaji na mikutano duniani kote. kwa taarifa zaidi, tembelea www.daghewardmills.org.

LanguageKiswahili
Release dateApr 7, 2018
ISBN9781641345408
Jinsi Unavyoweza Kutimiza Huduma Yako
Author

Dag Heward-Mills

Bishop Dag Heward-Mills is a medical doctor by profession and the founder of the United Denominations Originating from the Lighthouse Group of Churches (UD-OLGC). The UD-OLGC comprises over three thousand churches pastored by seasoned ministers, groomed and trained in-house. Bishop Dag Heward-Mills oversees this charismatic group of denominations, which operates in over 90 different countries in Africa, Asia, Europe, the Caribbean, Australia, and North and South America. With a ministry spanning over thirty years, Dag Heward-Mills has authored several books with bestsellers including ‘The Art of Leadership’, ‘Loyalty and Disloyalty’, and ‘The Mega Church’. He is considered to be the largest publishing author in Africa, having had his books translated into over 52 languages with more than 40 million copies in print.

Related to Jinsi Unavyoweza Kutimiza Huduma Yako

Related ebooks

Reviews for Jinsi Unavyoweza Kutimiza Huduma Yako

Rating: 5 out of 5 stars
5/5

1 rating0 reviews

What did you think?

Tap to rate

Review must be at least 10 words

    Book preview

    Jinsi Unavyoweza Kutimiza Huduma Yako - Dag Heward-Mills

    SURA YA 1

    Matukio Ya Kiungu Ambayo Hutimiza Huduma Yako

    Bali wewe, uwe mwenye kiasi katika mambo yote, vumilia mabaya, fanya kazi ya mhubiri wa Injili, TIMIZA HUDUMA yako kwa ukamilifu.

    2 Timotheo 4:5

    Inawezekana kutimiza huduma yako. Huduma ya Yesu Kristo ndilo jambo muhimu kabisa ambalo unaweza kuhusika nalo. Fursa kubwa kabisa ambayo imepewa binadamu ni kumfanyia kazi Mungu. Kumfanyia kazi Mungu kunaitwa 'huduma'. Ni jambo muhimu sana kwako kutimiza huduma yako. Ni jambo muhimu sana kwako ukamilishe kazi yoyote ambayo Bwana amekupatia hapa ulimwenguni. Usikae ufe kabla hujatimiza huduma yako.

    Hutafurahia kuwasili kwako mbinguni iwapo hukukamilisha huduma yako.

    Unafahamu inakuwaje kufanya mtihani ambao hukujitayarisha kufanya! Unafahamu inakuwaje wakati msimamizi wako anapokupata hujajitayarisha na huko tayari na kazi yako.

    Mwambieni Arkipo, Iangalie sana huduma ile uliyopewa katika Bwana, ili uitimize.

    Wakolosai 4:17

    Watu wengi wanasema kwamba hawajui wito wao ni upi, kando na kutojua jinsi ya kutimiza wito huo! Basi si zaidi sana kujua jinsi ya kutimiza huduma yao! Kitabu hiki kinahusu jinsi ya kutimiza huduma yako. Ikiwa unasoma kitabu hiki, basi wewe una huduma. Tambua onyo kali ambalo Paulo alitoa kwa Arkipo, Timiza huduma yako. Kwa maneno mengine, hakikisha umefanya na kukamilisha huduma yako.

    Watu wengi husema, Sina kipawa kama wewe na ofisi ya kiroho. Ukweli ni kwamba wengi wetu hawahisi kuwa na kipawa maalum cha huduma. Uhalisi wa mambo ni kwamba, wengi wametengwa na Mungu lakini hawaitikii wito huo. Watu wengi wameonyeshwa upendo lakini hawaitikii upendo huo.

    Ikiwa unafikiria utaona malaika kabla ya kuitikia wito wa Mungu, basi inawezekana usiitikie kamwe wito huo.

    Kuweza kutimiza huduma yako, lazima uelewe jinsi Mungu anavyokuita na kukuelekeza katika kuzaa matunda. Ili uweze kutimiza huduma yako, lazima uitikie matukio ya kiungu maishani mwako.

    Matukio ya Kiungu

    Watu wengi hawafahamu matukio yaliyopangwa na Mungu ni nini. Ukiwa unaelewa au la, kukosa kuitikia matukio ya kiungu ya maishani mwako kutahakikisha kwamba hutatimiza huduma yako. Watu wengi hawatimizi huduma zao kwa sababu hawaitikii matukio yaliyopangwa na Mungu ya maishani mwao. Matukio haya ya kiungu ni yapi? Matukio ya kiungu ya maishani mwako ni:

    1. Mvuto wa kiungu. (Yohana 6:44)

    2. Tamaa za kiungu. (1 Timotheo 3:1)

    3. Misimamo ya kiungu. (Yohana 16:7-8)

    4. Upendo wa kiungu. (Kumbukumbu la Torati 6:5)

    5. Huruma ya kiungu ya Mungu. (2 Wakorintho 4:1)

    6. Kutengwa kwa kiungu. (Kumbukumbu la Torati 10:8)

    7. Mapenzi ya Mungu. (Waefeso 1:9)

    8. Wito wa kiungu. (Warumi 1:1)

    9. Mwito wa kiungu. (Yona 1:1-3)

    10. Makusudi ya kiungu. (Mithali 16:4)

    11. Maono ya kiungu. (Matendo 26:19)

    12. Mgao wa kiungu wa vipawa. (Warumi 1:11)

    13. Neema ya kiungu. (2 Timotheo 1:8-9)

    14. Ofisi ya kiungu. (Warumi 12:4)

    Haina maana kujifanya kwamba unahitaji kusikia sauti halisi kabla ya kujua cha kufanya kuhusu huduma yako. Haina maana kudai kwamba unamngoja Yesu akutokee wewe kabla hujajua fanyika kile unachopaswa kufanya. Kuna matukio mengi ya kiungu ambayo yatakuongoza wewe kuelekea kwa huduma yako halisi na kukusaidia uitimize huduma hiyo.

    Mapenzi ya Mungu ya ajabu, kusudi la Mungu na Mungu kukuonyesha huruma, ni matukio ya nguvu yanayobadilisha maisha na ambayo yatakuelekeza moja kwa moja kwa huduma.

    Bila kuitikia huruma ya Mungu na upendo wa Mungu, huwezi kamwe kuwa katika huduma. Paulo alisema kwamba alishurutishwa na upendo wa Mungu. Utengano wako na familia yako, nchi yako na watu wako ni tukio muhimu la kiroho ambalo limefanyika maishani mwako. Kuitikia matukio haya ya kiroho kwa njia inayostahili kutakufanya wewe utimize huduma yako.

    SURA YA 2

    Fuata Yule Unayevutiwa Naye

    Hakuna mtu awezaye kuja kwangu, ASIPOVUTWA na Baba aliyenituma; nami nitamfufua siku ya mwisho.

    Yohana 6:44

    Fuata yule mtu unayevutiwa naye na utatimiza huduma yako! Kuvutiwa kwa mtu fulani ni jambo lisilokuwa la kawaida. Kuwa na hofu ya Mungu ndani yako na uwe na heshima halisi kwa yule ambaye Mungu anamuvutia kwako. Unapofuata wale watu unaovutiwa nao, utatimiza huduma yako!

    1. Ikiwa unavutiwa kwa Mungu, unakuwa na ufahamu usiokuwa wa kidunia.

    Kuvutiwa kwa Mungu ni jambo lisilokuwa la kidunia. Ni Baba anayekuvutia wewe. Watu wengi hawampendi Mungu! Watu wengi hawataki kuomba au kufunga. Watu wengi hawaipendi Biblia! Watu wengi hawapendi kanisa. Kuvutiwa kwa kitu ni kupendezwa nacho. Mungu huweka kitu hicho moyoni mwako ili uvutiwe kwake na kwa kanisa!

    Huenda ukajipata ukivutiwa kwa kanisa, kwa mambo ya Kikristo na kwa Mungu. Ni jambo la ndani kwa ndani kiasi cha kwamba hata huwezi kutambua kwamba unavutiwa kuelekea kwa kanisa na sio klabu cha usiku.

    Ni muhimu kutambua unachovutiwa nacho. Sisi sote tunavutiwa kwa vitu tofauti. Unapotambua kile unachovutiwa nacho, utaanza kutambua wito wako na unaweza kuanza kutimiza huduma yako.

    2. Ikiwa unavutiwa kwa mtu, pia unakuwa na ufahamu wa kiroho.

    Kuna utofauti gani baina ya kuvutiwa kwa mtu na kutamani kitu? Unapovutiwa kwa mtu fulani, utajipata ukielekea kwa huyo mtu. Unajipata ukiwa na shauku na kile ambacho mtu huyo anasema na kufanya. Unapotamani kitu, kuna uchu mkali wa ndani kwa kitu hicho. Hamu inatoa picha kubwa kabisa juu yako kuliko mvuto.

    3. Huenda ikawa vigumu kutambua wakati unapoanza kuvutiwa.

    Kuweza kutambua kile unachovutiwa nacho pengine ndilo jambo gumu kabisa la kiroho. Hii ni kwa sababu wakati unapovutiwa kwa Mungu, hutambui kile kinachofanyika kwako. Unajikuta tu uko kanisani, katika ushirika, kwenye mkutano na pamoja na wandugu.

    4. Utavutiwa kwa watu wa Mungu ambao Baba amechagua.

    Hakuna mtu awezaye kuja kwangu, ASIPOVUTWA na Baba aliyenituma; nami nitamfufua siku ya mwisho.

    Yohana 6:44

    Huenda ukavutiwa kwa mtu wa Mungu! Mungu atakuvutia kwa watu wale anaotaka ujifunze kutoka kwao. Watu wengi wa Mungu wanapendwa na baadhi ya watu na kudharauliwa na wengine. Mtu huyo huyo wa Mungu anayekufurahisha wewe huenda akakera watu wengine.

    Huenda ukapendezwa sana na mtu wa Mungu, ilhali mtu mwingine hawezi kuvumilia mtu huyo huyo. Hakuna awezaye kuja kwa Mungu asipovutwa na Baba. Mara nyingi Baba ndiye anayekuvuta kwake kwa njia isiyoonekana, isiyotambulika kupitia kwa mtumishi wake. Yesu alisema wazi wazi kwamba hakuna awezaye kuvutwa kwake Mungu asipofanyia kazi moyo wake na kumuvuta. Yesu hakufurahiwa au kupendwa na kila mtu. Wengi wa Wayahudi walitaka asulubiwe. Sio kila mtu alimchukulia kwamba alikuwa mtu mzuri. Yesu alielezea jambo hili kwetu aliposema, Hakuna mtu awezaye kuja kwangu, asipovutwa na Baba. Yesu alitambua kila mtu aliyevutwa kwake kwa sababu alijua kwamba lilikuwa si jambo la kawaida kwa mtu kuvutwa kwake.

    5. Utavutiwa kwa watu tofauti nyakati tofauti.

    Tena kesho yake Yohana alikuwa amesimama pamoja na wawili katika wanafunzi wake. Akamtazama Yesu akitembea, akasema, Tazama, Mwana-kondoo wa Mungu!

    Wale wanafunzi wawili wakamsikia akinena, wakamfuata Yesu.

    Yohana 1:35-37

    Katika huduma yako yote, Mungu ataweka ndani yako mvuto usioelezeka kwa watu ambao ni muhimu kwako kutimiza huduma yako. Ni muhimu kutambua mvuto usiokuwa wa kawaida wa Roho Mtakatifu. Kubali kwamba Roho Mtakatifu anakuvuta wewe kwa watu fulani.

    Hata wanafunzi wa Yohana walivutwa kwa Yesu waliposikia kumhusu yeye. Walimuacha bwana wao, Yohana Mbatizaji, na wakamfuata Yesu Kristo kuanzia siku ile waliyokutana naye. Yohana Mbatizaji aliridhika na hilo kwa sababu alijua kwamba yeye alikuwa mtangulizi tu wa kumtambulisha Yesu kwa ulimwengu.

    Katika huduma yangu yote, nimeona kuvutiwa na kuwa na shauku katika watu tofauti wa Mungu. Watu hawa wamekuwa muhimu sana kwangu kutimiza huduma yangu. Walishikiliana kila mmoja wao katika majukumu yao waliyochukua maishani mwangu. Nilivutiwa na Kenneth Hagin nilipokuwa tineja. Bado navutiwa na yeye hata ingawa nimefikia umri wa miaka hamsini. Nimevutwa pia kwa watu wengine wa Mungu katika majira tofauti ya maisha yangu. Watu hawa walikuwa na ushawishi mkubwa sana kwa huduma yangu.

    SURA YA 3

    Kubali Kukataliwa na Utimize Huduma Yako

    Alikuja kwake, wala walio wake HAWAKUMPOKEA. Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika

    Enjoying the preview?
    Page 1 of 1