Discover millions of ebooks, audiobooks, and so much more with a free trial

Only $11.99/month after trial. Cancel anytime.

Jivutie Upako
Jivutie Upako
Jivutie Upako
Ebook69 pages2 hours

Jivutie Upako

Rating: 0 out of 5 stars

()

Read preview

About this ebook

Hii kitabu ya kipekee na Dag Heward-Mills atawafundisheni nini maana ya kupata upako na jinsi gani unaweza kuwa mafuta kwa ajili ya huduma. Kujifunza jinsi ya kukamata upako kwa ajili ya kazi ya huduma. Kitabu hiki ni lazima kwa kila mhudumu.

LanguageKiswahili
Release dateJul 28, 2016
ISBN9781613953907
Jivutie Upako
Author

Dag Heward-Mills

Bishop Dag Heward-Mills is a medical doctor by profession and the founder of the United Denominations Originating from the Lighthouse Group of Churches (UD-OLGC). The UD-OLGC comprises over three thousand churches pastored by seasoned ministers, groomed and trained in-house. Bishop Dag Heward-Mills oversees this charismatic group of denominations, which operates in over 90 different countries in Africa, Asia, Europe, the Caribbean, Australia, and North and South America. With a ministry spanning over thirty years, Dag Heward-Mills has authored several books with bestsellers including ‘The Art of Leadership’, ‘Loyalty and Disloyalty’, and ‘The Mega Church’. He is considered to be the largest publishing author in Africa, having had his books translated into over 52 languages with more than 40 million copies in print.

Related to Jivutie Upako

Related ebooks

Reviews for Jivutie Upako

Rating: 0 out of 5 stars
0 ratings

0 ratings0 reviews

What did you think?

Tap to rate

Review must be at least 10 words

    Book preview

    Jivutie Upako - Dag Heward-Mills

    Sura ya 1

    Ni Lazima Upakwe Mafuta

    Sikupata mafunzo rasmi katika huduma, sikupitia shule ya Biblia na nilikuwa na mawasiliano kidogo sana na mtu mkuu wa Mungu yeyote. Wakati nilipoanzisha huduma, baadhi ya watu wa Mungu niliopata kufahamiana nao, waliishia kutilia mashaka na kupambana na wito wa Mungu katika maisha yangu. Sikuwa na mbadala kunyonya kwenye upako uliokuwa kwa watu wengine wa Mungu waliokuwa mbali kupitia kanda na vitabu vyao.

    Naamini kwamba nimepakwa mafuta na Roho Mtakatifu kusimama kwenye ofisi yangu ya huduma. Nina ushahidi mwingi sana unaonizunguka kutilia mashaka uhalisi wa upako katika maisha yangu. Pia naamini kwamba maendeleo ya kielekitroniki na kiteknolojia duniani ni kwa ajili ya faida ya ufalme wa Mungu na huduma. Teknolojia imefanya kuwa jambo linalowezekana kuwa karibu na watu ambao wamepakwa mafuta.

    Unaouhitaji ni Upako

    Wakati Mungu anapokuletea mtu wa Mungu, unapewa nafasi ya kumpokea na kujipatia upako ulioko kwenye maisha yake. Upako ni kitu kikuu ambacho wewe na mimi twakihitaji ili kufanya kazi ya Mungu. Nabii Zekaria alijua kuwa kitu muhimu zaidi kilikuwa ni upako. Ni yeye aliyesema, Si kwa uwezo, wala si kwa nguvu, bali ni kwa Roho yangu (Zekaria 4:6).

    Elisha pia alitambua kwamba kitu kilichofanya huduma ya Eliya kuwa yenye mafanikio kilikuwa ni upako. Wakati alipopata nafasi, aliomba upako. Baadhi ya watu wangeweza kuomba fedha, elimu au sifa alizokuwa nazo Eliya. Lakini Elisha alitaka upako tu!

    …Eliya akamwambia Elisha, Omba kwangu lo lote utakalo nikutendee, kabla sijaondolewa kwako. Elisha akasema, Nakuomba, sehemu mara dufu ya roho yako na iwe juu yangu.

    2 Wafalme 2:9

    Katika kitabu hiki, nataka nikushirikishe juu ya njia ya upako ambayo kwa kawaida huwa haiongelewi. Inaweza kuonekana mpya kwako, lakini ni halisi kabisa. Kama kuna njia yoyote ambayo unaweza kujipatia upako, tafadhali itumie! Siiwasilishi hii kama ndio njia pekee ambayo Mungu anaweza kukupaka mafuta; nakushirikisha tu kile nilichokipokea kutoka kwa Bwana. Nakushirikisha kile kilicho cha kibiblia na cha kimaandiko.

    Watu wengi wamepokea upako kwa njia ya kusikiliza kanda na kusoma vitabu, lakini hawaelewi kile kilichowatokea. Wengi wa wale waliopokea upako kupitia njia hii hawawezi kuifundisha kwa sababu hawaielewi kikamilifu. Naamini kwamba ni kazi yangu kuifundisha njia hii rahisi na halisi ya kujipatia kigezo muhimu zaidi cha huduma – upako.

    Sura ya 2

    Kuhusiana na Watu Wakuu  wa Mungu

    Katika kitabu kingine ¹, nimeshirikisha juu ya umuhimu wa kuhusiana kwa ukaribu na mtu wa Mungu ili kupokea upako ulio katika maisha yake. Kwa nini huna budi kuhusiana na watu wa Mungu waliopakwa mafuta? Ni nini hasa ukipatacho kwa kupitia uhusiano? Kwa kadri uhusianapo kwa ukaribu na mtu wa Mungu, utamsikia akizungumza mara kwa mara. Maneno haya yana upako. Wakati Elisha alipohusiana kwa ukaribu na Eliya, alimsikia yeye mwenyewe akizungumza mara kwa mara.

    Ikawa, walipokuwa wakiendelea mbele na kuongea…

    2 Wafalme 2:11

    Maneno Yana Nguvu!

    Yesu aliwaambia wanafunzi wake kwamba maneno yake yalikuwa na mambo mawili muhimu. Yalikuwa na uzima na Roho! Roho huyu ni yupi? Roho huyu ni upako! Maandiko husema kwamba Mungu alimpaka mafuta Yesu wa Nazareti kwa Roho Mtakatifu na kwa nguvu (Matendo 10:38). Yesu alipakwa mafuta kwa Roho Mtakatifu, na kwa hiyo Roho Mtakatifu (kitu ambacho kwacho alipakwa mafuta) ni upako.

    … maneno hayo niliyowaambia ni roho tena ni uzima.

    Yohana 6:63

    Kwa watu wengi, uhusiano wa karibu na watu wa Mungu tunaouzungumzia hauwezekani isipokuwa kwa kutumia njia ya vitabu na kanda. Vitabu na kanda vinaweza kuwa na maneno ya watu wa Mungu walipakwa mafuta. Maneno ya watu wa Mungu waliopakwa yana Roho na uzima.

    ¹ Tazama The Mega Church (Kanisa Kubwa), na Bishop Heward–Mills.

    Kujizamisha kwenye vitabu vilivyoandikwa na watu waliopakwa mafuta ni njia ifaayo sana ya kuhusiana nao. Muda unaotumia kusoma kitabu unatumiwa kushirikiana na mwandishi wa kitabu. Ni upendeleo ulioje kuwasiliana na mtu mkuu kwa masaa matatu mahali pa faragha nyumbani kwako!

    Wakati usomapo kitabu hiki unashirikiana nami na mimi nashirikiana nawe. Wakati niandikapo kitabu hiki, najisikia kwamba naongea na watu fulani. Nawahudumia moja kwa moja watu wengi watakaotoa muda [wao] kupokea. Kama Elisha alivyoyasikiliza maneno ya Eliya na wanafunzi walivyoyasikiliza maneno ya Yesu, unayasikiliza maneno yangu wakati usomapo kitabu hiki! Wanafunzi waliyasikiliza maneno ya Yesu; hivyo

    Enjoying the preview?
    Page 1 of 1