Sie sind auf Seite 1von 26

ZANZIBAR DAIMA ONLINE

www.zanzibardaima.net Toleo 04 - 2013

JARIDA LA KILA MZANZIBA R I

Septemba /Oktoba 2013

ZANZIBAR D A I M A ONLINE

Bakhressa apania uwekezaji

ZANZIBAR
Zanzibar

yaweza kusonga kwenye Soka

ZANZIBAR Y O U R D A I M A H NEL IRN E O

LO G O

Yaliyomo
JAR IDA LA KILA MZAN ZIBARI
www.zanzibardaima.net Toleo 04 - 2013

www.za

ics Graph er n g i Des ) saan .com (Hasa rim ge


nzib

Z anzibar Daima
J AR I DA LA KILA MZA NZIBA RI
www.zanzibardaima.net Toleo 04 - 2013

ZANZIBAR D A I M A ONLINE

Designer

HK

Online

Timu Yetu
TINDIKALI ZANZIBAR
MHARIRI MKUU Ahmed Rajab Email: ahmed@ahmedrajab.com MHARIRI MSAIDIZI Mohammed Ghassani Email: kghassany@gmail.com MHARIRI MSANIFU Hassan M Khamis Email: hassan@zanzibarimage.com COMMUNICATION MANAGER Hassan M Khamis

Bilionea wa Kizanzibari anayeurejesha utajiri kwao

SAID SALIM BAKHRESSA

06
Utitiri wa vijana wasio ajira waongezeka

12

WAANDISHI Jabir Idrissa Email: jabirgood@yahoo.com Othman Miraji Email: mwinjuu@hotmail.com Hamza Rijal Email: babujimba@hotmail.com Salim Said Salim Email: sssalim47@yahoo.com

NCHI IMEKALIA BOMU

Umuhali watuumiza Wazanzibari

WARAKA KUTOKA BONN

Mabunge mawili ya Muungano

HATUJAACHA KUSEMA

16 28
Inafaa na ni muhimu matamshi ya Kamishna Mussa yafafanuliwe na yaelezewe katika usuli mwema la sivyo yanaweza kuwa na hasara kubwa kwa Zanzibar, kwa sisi wenyewe kujiimbia nyimbo mbaya kuwa kumbe Al-Shabaab wameweza kufika Zanzibar

18 38
Mkristo akifa Zanzibar, Waislamu wanahudhuria mazikoni, na vivyo afapo Mwislamu. Wakristo wangapi Zanzibar wamekufa mikononi mwa Waislamu na Waislamu wakasimamia maziko yao kanisani mpaka wanashushwa makaburini

22 42
Haji Gora Haji ni mtu wa kisiwa cha Tumbatu, kaskazini magharibi karibu na Unguja. Tumbatu ina magofu ambayo, pamoja na Unguja Ukuu, ni ya zamani kuliko popote pengine huko Zanzibar,

Ally Saleh Email: allysaleh126@gamil.com WASAMBAZAJI mzalendo.net zanzibardaima.net zanzibardaima/facebook MATANGAZO Hassan M Khamis Simu: +44 7588550153 Email: hassan@zanzibarimage.com WASIALIANA NASI zanzibardaimaonline@gmail.com JARIDA HILI HUCHAPISHWA NA Zanzibar Daima Collective 233 Convent Way Southall UB2 5UH Nonnstr. 25 53119 Bonn Germany

www.zanzibardaima.net
UKURASA PAGE

Zanzibar Daima Online Toleo 04

3 03

UKURASA

ZANZIBAR Y O U R D A I M A H NEL IRN E O

LO G O

JAR IDA LA KILA MZAN ZIBARI


www.zanzibardaima.net Toleo 04 - 2013

TAHRIRI

J AR I DA LA KILA MZA NZIBA RI


www.zanzibardaima.net Toleo 04 - 2013

ZANZIBAR D A I M A ONLINE

Usiimwagie tindikali Zanzibar


H
Na Ahmed Rajab
amna shaka yoyote kwamba waliowashambulia watu Unguja kwa kuwamwagia tindikali kwa kipindi cha karibu mwaka sasa wamefanikiwa. Hawakufanikiwa kwa moja. Wamefanikiwa kwa mawili. Kwanza, kwa kuwadhuru waliowalenga. [Angalia Uk. 12] Pili, kwa kuidhuru Zanzibar. Washambulizi hao wameidhuru Zanzibar kwa sababu hawakuwamwagia tindikali waliowalenga tu bali pia wameimwagia tindikali Zanzibar yetu. Wakitaka, wasitake hiyo ndiyo athari walioiacha baada ya kuwamwagia tindikali hao waliowamwagia. Ndio maana tukaiona sura ya Zanzibar mbele ya ulimwengu ghafla imebadilika. Mashambulizi hayo yameifanya Zanzibar isawijike. Wajihi wake unachusha. Umejaa majaraha na makovu. Umefujika, umechafuka, umevurugika. Hautamaniki tena. Kwa hakika, unatisha khasa. Hivyo ndivyo baadhi ya walimwengu wanavyoiona Zanzibar siku hizi. Kuna wenye kuiogopa, hawataki
UKURASA PAGE

tena kuja kututembelea. Ingawa watalii bado wangali wakiendelea kuvizuru visiwa vyetu kwa mkururo, sekta ya utalii imepata mtikisiko kidogo kwa sababu kuna baadhi ya watalii kutoka nje ya Bara la Afrika waliovunja safari zao za kuja Zanzibar baada ya matukio ya karibuni ya mashambulizi ya tindikali. Pengine hiyo ndiyo iliyokuwa dhamiri ya washambulizi; kuukata miguu utalii visiwani mwetu. Na tukiyasema haya tusieleweke vibaya, kwamba labda tunazililia pesa mbili tatu zinazotutiririkia kutoka sekta hiyo. Tunachokililia ni kupoteza sharafu yetu na sifa yetu ya jadi ya kuwa watu wavumilivu, wapenda amani na wenye kuheshimu dini na imani za wengine. Tunachokililia ni jinsi mashambulizi hayo yalivyotumiwa kuuchafua na kuutia madoa Uislamu pamoja na ustaarabu wetu. Ni wazi kwamba serikali imeshindwa kufanya kampeni yoyote ile ya kuwaamsha watu kuhusu madhara ya mashambulizi kama haya kwa uchumi wetu na kwa jamii kwa jumla. Kwa hivyo, Zanzibar Daima Online ime-

jitwika dhima ya kuanzisha kampeni ya kutanabahishana Wazanzibari sote kuhusu madhara ya kujihujumu wenyewe kwa mashambulizi yasioingia akilini. Ni matumaini yetu kwamba asasi za kiraia, vyombo vya habari vya Serikali na vinavyomilikiwa binafsi, walimu maskulini na katika madrasa, wazee majumbani, mashekhe misikitini, vijana katika baraza zao, duru zao na vikao vyao pamoja na wadau wengine wataziunga

mkono juhudi za kuzinduana kuhusu uovu huu. Kaulimbiu yetu ni nyepesi: Tusiimwagie tindikali Zanzibar.

Sambamba na kampeni hii tunatoa wito kwetu sote katika jamii tuwe macho kuwaangalia wote wale ambao kwa vitendo vyao wataifanya Zanzibar iwe na jina baya. Vyombo vya habari vina dhamana ya kuwae- Hili si jukumu la mtu mmoja, la kikundi kilimisha wananchi kuhusu madhara na hasara moja, wala la chama kimoja. Hili ni jukumu inayopata nchi yetu kutokana na mashamletu sote. bulizi kama haya. Vinapaswa pia kuwashinikiza viongozi wetu wachukue hatua zinazo- Lazima tuhakikishe kwamba juu ya matahitajika kuzuia pasizuke tena mashambulizi tizo yote tuliyo nayo tunaendesha shughuli kama haya katika jamii yetu. zetu na harakati zetu zote kwa njia za amani. Lazima tuhakikishe kwamba tunaishi katika Jengine ambalo vyombo vya habari vinaweza mazingira ya usalama na utulivu. Lazima kufanya ni kuihimiza Serikali ifanye kampeni tuhakikishe kwamba tunaujenga Umoja yake ya kulisafisha jina jema la Zanzibar. wetu na Mshikamano wetu juu ya misingi ya amani.
UKURASA

ZANZIBAR Y O U R D A I M A H NEL IRN E O

LO G O

JAR IDA LA KILA MZAN ZIBARI


www.zanzibardaima.net Toleo 04 - 2013

Na Jabir Idrissa

Sasa Bakhressa aijenga Zanzibar


kusudia kubadilisha sura nzima ya usafirishaji abiria kwa njia ya bahari kutokea Zanzibar hadi Dar es Salaam na Zanzibar hadi Tanga kupitia Pemba. Baada ya kutokuonekana akielekeza nguvu za uwekezaji kwenye ardhi ya kwao, kwa siku za karibuni, Bakhressa ameshuhudiwa akifanya mengi visiwani Zanzibar yanayoashiria dhamira hiyo. la abiria kwenye Bandari ya mjini Zanzibar miezi miwili iliyopita, alisema pale anapotokea mwekezaji akataka kuwekeza fedha zake asisumbuliwe, asaidiwe. Wengine wanadhani, ukimya wa Bakhressa visiwani Zanzibar ulimaanisha hakuwa akifanya kitu kikubwa, ingawa inakumbukwa kwamba siku zote amekuwa mstari wa mbele, lakini chini kwa chini, kusaidia hapa na pale. Yumkini kwa sababu ya kutokupendelea kwake kujitokeza binafsi kwenye vyombo vya habari, ndio maana si mengi sana yanayojuilikana kuhusu jitihada hizo na hata za maisha binafsi ya Said Bakhressa. Lakini mtandao maarufu wa Wikipedia unasema Bakhressa alilazimika kuacha masomo akiwa na umri wa miaka 14 tu, alipojiingiza kwenye biashara ya kuuza urojo, chakula maarufu kinachouzwa visiwani Zanzibar nyakati za jioni na sasa unamtaja kuwa kigezo cha watu waliokwea ngazi za mafanikio ya kiuchumi kwa jitihada zake mwenyewe. Biashara yake ya kuuza chakula katika mitaa ya Dar es Salaam katika miaka ya 1970, ilikuja ikamuibua kuwa mmiliki wa himaya kubwa ya biashara ndani ya miongo mitatu baada ya hapo. Himaya yake imejichawanya kuanzia

HABARI KUU

J AR I DA LA KILA MZA NZIBA RI


www.zanzibardaima.net Toleo 04 - 2013

ZANZIBAR D A I M A ONLINE

arida la kibiashara linaloheshimika duniani, Forbes, linamtaja kama tajiri mkubwa kabisa wa Tanzania na kumuweka kwenye nafasi ya 30 kati ya matajiri wakubwa kabisa barani Afrika. Mtandao mashuhuri wa Wikipedia unamtaja kama tajiri aliyekwea ngazi mwenyewe kuelekea kilele cha mafanikio. Jina lake ni Said Salim Awadh Bakhressa, Mzanzibari aliyezaliwa mwaka 1949 na aliyejipatia sifa kama mwanaviwanda katika eneo hili.

Katika kufanikisha dhamira yao hiyo, Meneja Hussein anasema: Hatufanyi biashara Miongoni mwa kampuni leo kwa ajili ya leo. Hapana. zilizomo kwenye mtandao Biashara hii ukiingia unwake ni Azam Marine na Kili- abaki huko mpaka ufe na kile manjaro Fast Ferries za usafiri unachopata kama faida kinawa majini, ambayo meneja rudi kuimarisha miundombinu wake, Hussein Mohamed na maslahi ya wafanyakazi Said, anasema haijafikia kiwaliochangia mafanikio. wango hasa cha mafanikio inachotaka kukiona katika hu- Ndani ya kauli yake hiyo, anaduma za usafirishaji abiria na onesha upande wa Bandari ya mizigo kwa njia ya baharini. Dar es Salaam, pembeni mwa ofisi kuu za kampuni hiyo amTunakusudia kuweka nguvu bako mahojiano na mwandiPemba na Tanga. Unajua shi wa Zanzibar Daima Online kule Mkoani (Pemba), Banyalifanyika. darini vyombo vinafunga gati kwenye ukuta badala ya gati Meneja Hussein anaulizwa nzuri. Tunataka tufunge gati sababu za uwekezaji mkubwa kama tunavyofunga hapa Dar kufanywa kipindi hichi. Tulies Salaam na kama tunavyo- kusudia muda mrefu kuwekefunga pale nyumbani Zanziza, lakini vikwazo vilikuwa bar, anasema. vingi. Hussein maarufu kwa jina la Meneja Hussein, anasema Azam Marine pamoja na Kilimanjaro Fast Ferries, wameUKURASA PAGE

Anakumbusha maneno ya Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein ambaye alipozindua eneo jipya na la kisasa

SAID SALIM BAKHRESSA

UKURASA

ZANZIBAR Y O U R D A I M A H NEL IRN E O

LO G O

JAR IDA LA KILA MZAN ZIBARI


www.zanzibardaima.net Toleo 04 - 2013

HABARI KUU
mtu alikwenda kuomba kuwekeza akakataliwa? Sisi ndio tulipata wazo baada ya kuona hali inavyozidi kuwa mbaya. Tukaenda serikalini kujieleza. Tukataka ruhusa hatimaye tukasaidiwa kutekeleza azma yetu. Kupitia uwekezaji wa Azam Marine na Kilimanjaro Fast Ferries, kumejengwa eneo la kisasa la abiria bandarini Zanzibar ambako watu wapatao 600 wanakaa wakati wakisubiri kusafiri. Meneja Hussein hapendi kutaja kwa uhakika thamani ya uwekezaji huo. Tumetumia kama shilingi bilioni mbili hivi. Kwa upande wa eneo la abiria bandarini Dar es Salaam, ametaja gharama nusu ya hizo. Anasema wamewekeza pia kwa sababu wamegundua nini abiria wanakitaka. Abiria wanataka kusafiri kwa raha. Wanataka kuona mandhari wakiwa ndani ya boti, wengine wakiwa nje wamekaa, mbele au nyuma ya chombo. wapi madogo. Anatafiti namna ya kujenga chombo kitakachokuwa salama. Hapo inakuwa kazi rahisi kutujengea chombo kinachofaa mazingira ya watu wetu, anasema.

J AR I DA LA KILA MZA NZIBA RI


www.zanzibardaima.net Toleo 04 - 2013

ZANZIBAR D A I M A ONLINE

kwenye vyakula na vinywaji hadi usafiri wa baharini na viwanda vya kusindikia nafaka na maziwa, na hivi karibuni mradi mkubwa wa vyombo vya habari, akianzia na televisheni ya Azam TV. Timu machachari ya mpira wa miguu nchini Tanzania, Azam FC, inamilikiwa na makampuni haya. Dk. Shein anayesemekana kuongoza mwenyewe msukumo wa Serikali katika kufanikisha dhamira ya Azam Marine ya kuwekeza eneo hilo, alisema ameshangazwa na mitizamo dhaifu ya watendaji wa taasisi za kusaidia wawekezaji kutumia fursa za kuwekeza.

tuliyokubaliana. Tukaamua kuacha lakini tukiumia sana kwa sababu kila mtu anajua hali ya bandarini ilivyokuwa mbaya, anasema Meneja Hussein. Bila ya kuficha, anakiri hali hiyo ilitokea wakati wa Serikali ya Awamu ya Sita (SAS), chini ya Amani Abeid Karume. Rais hakuwa tatizo. Tatizo ilikuwa watendaji wizarani na kule Bandari. Unakuta wanaogopa hata kufanya majadiliano. Tunashukuru safari hii tumepata ushirikiano mzuri ndio maana unaona kazi imefanyika. Wamebadilika kama alivyowahimiza Dk. Shein.

Mtu anakuja na pesa zake, anataka kuwekeza eneo Anakiri hakukuwa na zabuni fulani, mnamsumbua weee mpaka anachoka anaondoka. lakini anahoji kwani kuna Hatuwezi kwenda namna hiyo mjuwe mwenye pesa ana sehemu nyingi za kutumia pesa zake. Badilikeni viongozi nyie. Muwe wepesi wa kumsaidia mtu kama huyu bila ya kukiuka taratibu, Dk. Shein alisema. Tunaambiwa kumbe Azam Marine walikuwa na majadiliano siku nyingi na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar yaliyohusu kuruhusiwa kujenga eneo la kisasa la abiria bandarini lakini woga na urasimu uliwakwamisha. Tulikuwa na ndoto hii zamani. Tukafanya mazungumzo mara nyingi na viongozi wa serikali lakini kila tulipomaliza hatukuona maendeleo ya mambo
UKURASA PAGE

Meneja Hussein anatoa kisa cha mama ambaye licha ya Ndio maana tunatengenekulipa tiketi za daraja la juu, zesha boti kwa kuzingatia amekataa kukaa panapohimahitaji hayo ya wasafiri. tajika. Aliamua kukaa chini, Tunamwita mchoraji na kuwatoto wake wakakaa nje muelekeza chombo kiwe vipi. wapunge upepo. Pale kweWapi pakae viti vya abiria, nye viti vya VIP ameweka tu vingapi; wapi pakae vyoo, mabegi yake, yeye amekaa vyoo viwe vya kubonyeza au apendako. kuvuta. Anachoeleza hapa, abiria Designer wetu kutoka Aus- wengi wanapenda kukaa tralia alikuja tukampeleka nje zaidi kuliko ndani ya mpaka Pemba na Tanga kuboti wakati wa safari. Hata ona mwenyewe. Ameangalia watalii, hawapendi kukaa ukubwa wa bahari, nguvu za ndani ya boti. Wanataka kumawimbi. Wapi makubwa, ona kila kitu kizuri kwa karibu huku wakipiga picha.

Tanga. Tunataka ile picha halisi ya nchi yetu aipate kupitia safari yake. Lazima umpumbaze mtu kwa kumuonesha kizuri unachoweza kumpatia. Zamani ilikuwa vigumu. Hatukufanikiwa kuwavuta watu. Meneja Hussein anasema leo, wasafiri wengi wa Zanzibar kutokea Dar es Salaam wanatumia boti. Hata alipobanwa kufafanua kwa vile kwa boti mtu anatumia muda zaidi kuliko ndege, anasema: Tupo katikati ya jiji. Mtu akifika akiwahi chombo cha muda huo anaondoka. Hii ni kitu cha dakika 15. Akitumia saa mbili baharini anaona mambo mengi, anapata kuona mandhari, anaiona nchi kutoka baharini. Sasa inachukua saa moja na zaidi kufika Airport. Tena unatakiwa kuripoti saa mbili kabla ya muda wa kusafiri. Ukifika uwanja wa ndege Zanzibar, utafute gari ya kukupeleka mjini. Huku ukishuka tu boti, upo mjini. Hii ndiyo tafauti kubwa ya safari hii moja kwa njia mbili.

Afisi ya Uhamiaji bandarini Zanzibar, seheme ya jengo jipya lilojengwa na Said Bakhressa

Haya yametusukuma kubuni mfumo mpya wa kupata vyombo vya kisasa. Ni tofauti na ilivyo kwa wenzetu. Kwetu ni joto si baridi kama Ulaya, anasema Meneja Hussein kuhusu nini hasa Anasema kwa baharini, abiria kinavutia wao kupata ana uchaguzi saa moja asuvyombo vya kisasa. buhi, saa 3.30 asubuhi. Saa 6 mpaka 7 mchana. Na chomAlipoulizwa ni kwa bo cha mwisho ni saa 9.45. nini wanadhani Chombo kikiondoka, una saa muhimu kujua mambili umefika uendako. Hii hitaji ya watu wandiyo njia nzuri kabisa kwa naosafiri, anasema anayetaka kwenda Zanzibar Kwanza tumeamua na Pemba. kumvuta mtu aje kutumia usafiri huu Asiyejua utamu wa kwenda kwenda Zanzibar, Zanzibar kwa boti, aulize Pemba na baadaye wageni na watalii. Wao
UKURASA

ZANZIBAR Y O U R D A I M A H NEL IRN E O

LO G O

JAR IDA LA KILA MZAN ZIBARI


www.zanzibardaima.net Toleo 04 - 2013

HABARI KUU

J AR I DA LA KILA MZA NZIBA RI


www.zanzibardaima.net Toleo 04 - 2013

ZANZIBAR D A I M A ONLINE

BOTI MV KILIMANJARO INAYOSAFIRI BAINA YA DAR ES SALAAM, UNGUJA NA PEMBA

wakisafiri hawatulii, kila dakika wanapiga picha. Wanaona mambo ya ajabu baharini kwa karibu na kwa mbali kutokea kwenye boti. Hiyo tisa, waangalie boti inapokaribia kufika Zanzibar. Wanaona mambo kwa karibu zaidi basi kila mmoja anashughulika kupiga picha. Na hizi ndio raha wanazozitaka ambazo kwao haziko. Meneja Hussein anasema ushindani hauwasumbui kwa sababu wao wanatoa huduma zinazomvutia kila mtu.Ushindani upo lakini sisi tunajua abiria wanachokitaka. Tuna vyombo vizuri vya kisasa. , lakini si kampuni pekee kwenye mtandao wa makampuni unaomilikiwa na mfanyabiashara huyu wa Kizanzibari, Said Bakhressa, ambaye k wa mujibu wa mtandao wa Wikipedia, yeye mwenyewe ndiye kiini cha mafanikio yote hayo ya makampuni yake, kupitia dira yake na stadi zake binafsi za ujasiriamali na usimamizi wa miradi anayoianzisha.
UKURASA PAGE

Kwa mujibu wa jarida la Forbes la mwaka 2012, utajiri wa Bakhressa ni sawa na dola milioni 520 na yumo kwenye orodha ya matajiri wakubwa kabisa 40 barani Afrika. Nchi jirani ya Tanzania, kama vile Rwanda, zinategemea unga unaozalishwa na viwanda vya Bakhressa ambapo hupokea tani 120,000 za unga wa ngano na mahindi kwa mwaka, kiwango kinachopunguza makali ya kupanda bei za vyakula kwenye nchi ambayo asimilia 52 ya familia zake hazina uhakika wa kupata chakula chao. Kwa mujibu wa Mkakati wa Usaidizi wa Nchi uliobuniwa na Benki ya Dunia, hili ni jambo lenye manufaa sana. Vile vile, miradi ya Bakhressa nchini Rwanda inatarajiwa kuunda nafasi za ajira na kusaidia mapato ya nchi hiyo yatokanayo na kodi ya makampuni. Nchini Tanzania, Bara na Zanzibar, makampuni ya Bakhressa yameajiri watu wapatao 2,000 na yanatajwa kuwa makampuni makubwa kabisa kumilikiwa na kuendeshwa na mzawa kwa asilimia 100. Jina lake la Azam ni alama ya mtengenezaji mkubwa wa chokoleti na malai nchini Tanzania.

Kampuni yake ya vinywaji, zikiwemo sharubati, soda na maji, ina uwezo wa kuzalisha tani za ujazo 2,100 kwa siku na mwaka 2011 iliuza bidhaa zenye thamani ya dola milioni 800. Kitengo chake cha usafiri wa majini, Azam Marine, kinatoa usafiri wa hadhi ya kitalii ndani ya Tanzania. Nje ya miradi ya kibiashara, Bakhressa anajihusisha na miradi ya kijamii kama vile mradi wa kupunguza athari za ugonjwa wa malaria kwa wafanyakazi wake na kuzuwia kusambaa kwa maradhi kwenye maeneo yake ya kazi. Matokeo yake, kampuni yake hutumia dola 3400 tu kwa mwezi kwa ajili ya matibabu ya malaria kinyume na dola 10,000 za kuwatibu waajiriwa wake wanaouguwa. Wafanyakazi wake waliacha kutumia madawa aina ya Fansidar na kutumia madawa mchanganyiko, ambapo makampuni mengine nchini Tanzania yanatajwa kuungana na Bakhressa Group katika kampeni ya kupambana na malaria kwenye eneo la Afrika ya Mashariki na Kati. Hata wakaazi wengine nchini Tanzania wanaofanya kazi nje ya kampuni za Bakhressa wanafaidika na vita vya kupambana na malaria vya kampuni hiyo barani Afrika.
UKURASA

10

11

Zanzibar inapomwagiwa tindikali

ZANZIBAR Y O U R D A I M A H NEL IRN E O

LO G O

JAR IDA LA KILA MZAN ZIBARI


www.zanzibardaima.net Toleo 04 - 2013

NGURUMO LA MKAMANDUME
jambo hilo. Kwa ujumla, namna unavyolitazama jambo kwa jicho la ndani, ndivyo pia unavyolipokea kwa mikono ya ndani. La mashambulizi ya tindikali visiwani Zanzibar nalo linaangukia kwenye mitazamo kwa: ikiwa si kwa wayafanyao na wafanyiwao, basi angalau kwetu sisi tuyatafsiriyo. Ndio maana ndani yake kuna mitazamo mingi tafauti kutoka kwa watu wengi tafauti. Kundi moja la watu linayatazama mashambulizi haya kwa mtazamo wa kidini. Nitaliita tindidini. Hawa wanasema mashambulizi haya yanafanywa na Waislamu wa Kizanzibari wenye chuki dhidi ya dini nyengine, hasa Ukristo. Kanisa, vyombo vya habari vya ndani na nje na, kwa hakika, hata vyombo vya dola vimekokotwa na mtazamo huu. Kwa sababu ya mtazamo huo, hivi sasa polisi ya Zanzibar imetoa ile ninayoiita kadi ya mwaliko kwa kundi la kigaidi la al-Shabaab, kupitia kauli ya Kamanda Mussa Ali kwamba eti miongoni mwa waliokamatwa mwishoni mwa wiki wakiwa na tindikali, wamo waliosema walikuwa njiani kwenda Somalia kuwasaidia al-Shabaab. Tindikali haijawahi kuwa mbinu ya makundi ya kigaidi kokote duniani. Kimsingi wapambanaji wao wanaamini juu ya kupambana kwa kujitoa mhanga, yaani kuitumia miili yao kama silaha kuwadhuru wengine. Lakini kusema haya hakuondoshi ukweli kwamba

J AR I DA LA KILA MZA NZIBA RI


www.zanzibardaima.net Toleo 04 - 2013

ZANZIBAR D A I M A ONLINE

mwelekeo, tabia, matendo na maelezo ya kundi hili la wanatindidini yamo ndani ya duara hilo la dini.

Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, akimpa pole Sheha wa Shehia ya Tomondo, Unguja, Mohamed Omar Said (Kidevu), aliyeshambuliwa wa tindikali na watu wasiojuilikana mwezi Mei 2013

Mtazamo wangu ni kwamba kuendelea kwa mashambulizi kama haya ni kielelezo cha uwezo mdogo wa jeshi la polisi kiintelijensia na kitaalamu, kwani licha ya kuwa ni la Muungano, Zanzibar jeshi hili limezoea kutumikia siasa tu. Na Mohammed Ghassani
Mtazamo ni neno dogo lakini kubwa. Udogo wake umo kwenye wepesi katika mazungumzo ya kawaida. Kwa mfano, unapohitalifiana na mwenzio huwa mwepesi wa kusema: Lakini huo ni mtazamo wako tu. Mimi sijakusudia hivyo! Nalo likabaki kuwa
UKURASA PAGE

Kuna mtazamo mwengine unaosema kwamba mashambulizi haya ni uhalifu wa kawaida unaotokana na visasi vya ama kitaasisi, unyumba na au biashara. Kwao ni sadfa tu kuwa miongoni mwa waliolengwa ni viongozi wa kidini, Sheikh Wazanzibari wenzangu wenSuleiman Soraga na Padri An- gi wanaamini nadharia hii ya selm Mwangamba. hujuma. Kwa jicho la ndani ndivyo wayaonavyo mashamNdio maana huko nyuma ku- bulizi haya na kwa mikono ya likuwa pia na Mkurugenzi wa ndani ndivyo wayapokeavyo. Manispaa, ambaye si kiongozi Mwelekeo, tabia na maelezo wa dini. Ndio maana kuna pia yao yamo ndani ya duara hilo wasichana wadogo wa Kiin- la hujuma. gereza, ambao hawakuwapo Zanzibar kwa sababu za kidini. Lakini mimi nataka nitafauWenye mtazamo huu huse- tiane nao juu ya nani anatuhuma hata viongozi wa Kikristo jumu. Nayatazama matukio waliokumbwa na masham- haya kupitia jicho la uwezebulizi haya na mengine ni kano wa visasi au uhalifu Wakatoliki tu. Mwelekeo, ta- mwengine na sio hujuma bia na maelezo ya kundi hili kwa nchi wala serikali yetu ya yamo kwenye duara la kwam- Umoja wa Kitaifa. Naamini kila ba hii ni kazi ya ndani. tukio linajitegemea. Mtazamo wa tatu ni wa hujuma dhidi ya Zanzibar. Huu una mbeya mbili kisiasa na kiuchumi. Kisiasa, wanasema inayolengwa hapa ni, kwanza, Serikali ya Umoja wa Kitaifa, na pili ni ajenda ya Zanzibar kuelekea mamlaka kamili. Kwa kuwa kwa mara ya kwanza Wazanzibari wameweza kupaza sauti zao kudai nafasi kubwa ndani ya Muungano, jambo ambalo linaonekana kuwezeshwa na mfumo wa serikali uliopo, basi njama zinafanyika kuikwamisha serikali na, hivyo, hatimaye kuikwamisha ajenda hiyo.

Kiuchumi, wanahujuma, wanasema unaokusudiwa kuhujumiwa hapa ni utalii, ambao ndio uti wa mgongo wa uchumi wa Zanzibar. Wageni hawatavutiwa na pahala ambapo mashambulizi kama haya yanafanyika. Sekta ya utalii itaporomoka na serikali itashindwa kupokea mapato yatokayo nao.

hivyo mtazamo sio ukweli mengi, kwani namna unavyowa mambo. litazama jambo kuna maana kubwa kwa mwelekeo wa kuUkubwa wake upo kwenye liendeleza jambo hilo na hatiuhalisia, kwani mtazamo ni maye matokeo yake. namna unavyolitazama jambo kwa jicho la ndani na sio la Tafsiri yako ya mtazamo hunje tu. Waswahili waliposema zaa tabia zako, matendo yako jicho si mboni walipatia kwa na hata maelezo yako juu ya

Mashambulizi ya tindikali Zanzibar si mageni. Yalikuwapo hata kabla ya kuundwa serikali hii ya sasa. Nakumbuka mikasa ya huko nyuma iliyoambatana na siasa za kuripuliwa mabomu ya petroli kwenye taasisi za umma au nyumba za mawaziri kila ukikaribia au ukimalizika uchaguzi. Lakini mengi ya mabomu hayo yaliishia kuharibu mabanda ya kuku au milango tu. Na hata uchunguzi ulipofanywa na wataalamu kutoka Bara, uliishia kwenye ripoti zilizofichwa hadi leo, pengine kwa kuwa vidole vya ushahidi vilielekea kule ambako
UKURASA

12

13

ZANZIBAR Y O U R D A I M A H NEL IRN E O

LO G O

JAR IDA LA KILA MZAN ZIBARI


www.zanzibardaima.net Toleo 04 - 2013

NGURUMO LA MKAMANDUME

J AR I DA LA KILA MZA NZIBA RI


www.zanzibardaima.net Toleo 04 - 2013

ZANZIBAR D A I M A ONLINE

WASEMAVYO WANAFACEBOOK

N
Padri Anselm Mwangamba wa Kanisa Katoliki Zanzibar alishambuliwa kwa tindikali na watu wasiojulikana wiki iliyopita Mjini Unguja. wakubwa wasingelitaka vielekee, au nyumbani. kwa kuwa haukuwa uchunguzi jambo. Lakini ni nani hao tunaowapeleka Moshi na wana sifa gani kielimu? Mtazamo wangu ni kwamba kuendelea kwa mashambulizi kama haya ni kiele- Taaluma ya kompyuta inatufundisha lezo cha uwezo mdogo wa jeshi la polisi kanuni ya GIGO - yaani Garbage In, Garkiintelijensia na kitaalamu, kwani licha bage Out. Tukipanda michongoma, tutaya kuwa ni la Muungano, Zanzibar jeshi vuna chongoma. Askari polisi waliopata hili limezoea kutumikia siasa tu. kazi kwa mirengo yao ya kisiasa wanajua tu kutumikia mirengo hiyo na siyo Mtazamo wangu ni kwamba tunajihuju- taaluma ya upolisi. mu wenyewe kwa kuwa na jeshi la polisi lenye kiwango tulichonacho. Hawa hawataweza kuwalinda wenyeji na wageni na mali zao. Wataweza tu Wala pasisemwe kwamba hii ni taasisi kuulinda mfumo wa kisiasa uliowapa ya Muungano na sisi hatuna dhima yetu ajira zao. katika, kwa mfano, askari wangapi na wenye uwezo gani wawepo Zanzibar. Hata hivyo, ukweli ni kwamba katika Tunayo dhima hiyo. mashambulizi haya ni Zanzibar inayomwagiwa tindikali. Ni Zanzibar inayoNi sisi tunaopeleka majina ya nani na tendewa uhalifu huu kama nchi na kama nani waingie Chuo cha Polisi Moshi. Asil- taifa. imia kubwa ya hao hurudi kufanya kazi

alaani vikali kitendo cha kumwagiwa tindikali kwa Padri Joseph Mwangamba kilichotokea mchana wa siku ya Ijumaa ya tarehe 13 Septemba 2013 huko Mlandege, Zanzibar. Kwa kweli ni kitendo cha kinyama kisichoendana na mila na desturi zetu za Kizanzibari zinazofuata misingi na mafundisho ya dini yetu ya Kiislam na ni kitendo cha uvunjifu wa haki yake ya kuishi kwa salama na amani bila bughudha yoyote. Kuna mengi ya kujadiliana juu ya masuala kama haya yenye kuhatarisha mustakbali wa amani yetu na maisha yetu kwa ujumla. Nakubaliana na baadhi ya wenzangu wenye mtazamo wa kuwa wengi wa polisi wetu inavyoonekana huwa wanasainiwa na kupelekwa masomoni bila ya kuangaliwa ama kupimwa viwango vyao vya kielimu, bali kwa kujuana ama kwa ushawishi wa kisiasa. Hivyo utendaji wao wa kazi tunauona kuwa si wa kuridhisha kabisa kila siku zikienda. Tuje kwenye hili tatizo la kumwagiwa tindikali. Ni lazima tuangalie kila aina za uwezekano juu ya tatizo hili, kwanini limekuwa linatokea mara kwa mara hususan siku za hivi karibuni huko nyumbani Zanzibar? Wako watakaoshuku kuwa inawezekana ikawa ni hujuma dhidi ya Wazanzibari waonekane ni watu wenye ubaguzi wa kidini hasa katika kipindi hichi cha kudai mamlaka kamili ya Zanzibar, ili wasipate kuungwa mkono na mataifa ya Magharibi juu ya lengo lao hilo. Inawezekana ni mipango ya kundi la watu fulani wenye malengo fulani tusiyoyatambuwa

ambao wanatutumia ujumbe, lakini tunashindwa kuufahamu. Inawezekana ni wahalifu waliozoeleka wakiwa kwenye shughuli zao za kihalifu. Inawezekana ni watu wanaojuana wenye visasi vya siku nyingi, wanalipiziana. La kufanya ni kuliimarisha jeshi letu la polisi kwa kulipatia vitendea kazi vya kisasa na mafunzo imara na ya mara kwa mara kwenye utaalamu wa kisasa wa kisayansi na kiintelijensia ili kuweza kufanya kazi zao vyema. Vile vile, kuhimiza ushirikiano mzuri ulio wa kuaminiana na usio na vitisho baina ya polisi na raia wa kawaida katika jamii yetu. Jeshi la polisi nalo liache upendeleo wa kutumikia chama tawala na badala yake lifanye kazi zake bila upendeleo kwa kuzingatia haki na usawa ndani ya jamii ili wananchi warejeshe imani kwa jeshi hilo na wawe tayari kushirikiana nalo katika kuzuia vitendo vya kihalifu na pia kuwafichua wahalifu wanapofanya vitendo vya kihalifu. Kwa kweli tukiweza kufanya hayo, basi tutaweza kupiga hatua nzuri na za kuridhisha sio kama ilivyo hivi sasa kwani jeshi letu la polisi limekosa imani ya wananchi na hivi sasa linaonekana halifanyi kazi zake kwa ufanisi wa kutosha na kuridhisha kwani vitendo vya kihalifu na kinyama kama kumwagiana tindi kali vinazidi kuongezeka na watenda uhalifu huo wamekuwa wagumu kupatikana na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria. Lazima tutafakari ama sivyo tutaishia pabaya. Mimi, Haji Jingo
UKURASA

UKURASA PAGE

14

15

ZANZIBAR Y O U R D A I M A H NEL IRN E O

LO G O

JAR IDA LA KILA MZAN ZIBARI


www.zanzibardaima.net Toleo 04 - 2013

WARAKA MAALUM

J AR I DA LA KILA MZA NZIBA RI


www.zanzibardaima.net Toleo 04 - 2013

ZANZIBAR D A I M A ONLINE

Na Mustafa Sharif

Nchi yetu imekalia bomu


mazingira ya kuwafanya waripuke siku ustahamilivu utakapowashinda. Likitokea hilo sijui kama tutakuwa na uwezo wa kuwazuia maana watakuwa wengi na wenye hasira, waliokata tamaa na wasiosikia tena maneno tunayowaambia sasa ya kuwapoza na kuwatuliza. Mifano mengi tumeiona ya jinsi vijana walivyoripuka kuanzia Tunisia, Libya, Misri na kwengineko duniani. Mengi miongoni mwa haya yametokana na vijana kukosa imani na viongozi wao ya kwamba hawapo kwa ajili ya kusimamia maslahi yao na kuwatengenezea fursa za kuishi maisha bora, hivyo inapofika wakati huona bora litote ili ijulikane mbichi na mbivu. Siombi tufike huko ila ninachokiomba ni kwa viongozi wetu waweze kuliona hili la vijana kukosa ajira kama ni bomu la masaa au kijanga cha moto kinachochezewa kwenye mafuta na kutafuta njia ya kuyaepusha makubwa yasitokee.
UKURASA

ijana wa nchi hii kama vijana wengine kwengineko duniani wamekuwa wakipuuzwa na kuimbiwa nyimbo ambayo sasa wameshaanza kuchoka kuisikia. Kila nikikaa na kutafakari naona vijana wengi miongoni mwetu huchoshwa na hali ya kutokuwa na ajira au njia za kuweza kujipatia kipato na kuendeleza maisha yao na familia zao. Kubwa linalonitisha mimi ni hili suala la kuona utitiri wa vijana ambao hawana ajira wakiwa wamezagaa mitaani bila ya kuwa na la kufanya wala mwelekeo mahsusi wa Bila ya shaka ni kweli kwammaisha yao ya sasa na baa- ba kwa sasa hali ya kiuchumi daye. ni duni nchini kwetu na serikali yetu haiwezi kumuaHali si shuwari kiasi cha jiri kila kijana ambaye yuko kwamba tukiacha wale am- tayari kupatiwa ajira, lakini bao walikosa au walikataa kuna mengi mengine amfursa ya kujitafutia elimu na bayo yanachangia kwa kiasi hivyo kukosa vigezo vya ku- kikubwa kukuza tatizo hili la weza kuajiriwa imefika hadi ukosefu wa ajira. wale ambao wameweza kusoma na kufikia viwango vya Msemo wa kiingereza wa juu vya elimu nao huwawia it does not matter who you vigumu kuweza kupata ajira know but what you know kwa hata katika zile fani ambazo maana ya kwamba haijaliwana utaalamu nazo. shi nani unayemjua bali nini unachokijua umegeuzwa

sasa na imekuwa it does not matter what you know but who you know yaani haijalishi unachokijua bali nani unayemjua kwani fursa za ajira zimekuwa zikitolewa kwa kujuana tu, watu wanapeana kazi kimjomba mjomba na hizo kazi zenyewe zinafanywa kimjomba mjomba. Wale wenye utaalamu na wanaostahiki kupewa hizi nafasi hakuna anayewauliza au hata wakiulizwa kitu kidogo nacho kitembee. Serikali na jamii kwa ujumla

zimekuwa zikilaumiwa kwa kutofanya juhudi za maksudi za kutoa fursa ambazo zinaweza kuwapatia vijana wengi ajira na kuwaondoa mtaani ili wasije wakaleta majanga kwao na kwa taifa kwa jumla.

kuwajengea uwezo wa kubuni njia za kujiajiri wenyewe na hatimaye kuondokana na tatizo la ukosefu wa ajira.

UKURASA PAGE

Vijana wamekuwa miaka mingi madarasani bila ya kufundishwa mbinu mbadala Elimu yetu iitwayo ya bure za kuweza kujiajiri na kuajirini bure kwa maana haina wa katika sekta mbali mbali thamani na sio tu kwamba za kiuchumi. haipatikani kwa pesa. Elimu wanayopatiwa vijana wetu Tunapokosa kupanga miimekuwa haiwawezeshi ku- pango madhubuti ya namna wapa ujuzi ambao wanawe- gani tunaweza kuwapatia za kuutumia katika ushinda- shughuli za kujishughulini wa soko la ajira au kuweza sha vijana wetu, tunaandaa

16

17

ZANZIBAR Y O U R D A I M A H NEL IRN E O

LO G O

JAR IDA LA KILA MZAN ZIBARI


www.zanzibardaima.net Toleo 04 - 2013

Umuhali unatuumiza Wazanzibari

WARAKA KUTOKA BONN

J AR I DA LA KILA MZA NZIBA RI


www.zanzibardaima.net Toleo 04 - 2013

ZANZIBAR D A I M A ONLINE

Biashara ya holela holela imekuwa sehemu ya maisha ya Wazanzibari licha ya miaka kadhaa ya historia ya biashara ndogondogo na kubwakubwa ya visiwa hivi vya Bahari ya Hindi. Uholela na umuhali unayarudisha nyuma maisha kwa kiasi kikubwa bila ya watu kujijua.

Na Othman Miraji
karibu na nuksani kwa maendeleo yetu sote, kwani umejipenyeza pia hata katika mfumo wa namna tunavyoendesha masuala ya kiutawala. jNiliwahi kuhudhuria mazishi Unguja. Ilipomalizika sala ya maiti msikitini niliingiwa na shauku kutaka kulisindikiza jeneza hadi makaburini, Mwanakwerekwe. Hakujakuweko teksi ya kunipeleka. Watu hapo waliniambia sina Wajerumani wana neno haja ya kupoteza pesa kwa moja Unangemessen lenye maana karibu sawa teksi. Niliongozwa hadi katika moja ya magari ya serikali na muhali, japokuwa wao wanao kidogo na wanaupiga yaliowaleta watu mazikoni. vita. Wao huzungumia kama Lilikuwa lori, nilipanda, na pamoja na magari mengine vile kutumia vibaya nafasi yaliongozana hadi makabuau cheo chako na kupinda kanuni zilizowekwa ili ujipa- rini. Kurejea nilifikishwa hadi mlangoni nyumbani. tie faida ya kitu, umaarufu, Nilimuuliza dereva kiasi gani heshima na kupendwa na watu, licha ya kwamba athari malipo ya usafiri. Alinijibu: Wacha nishai Mzee. Hii si zake ni mbaya kwa maslahi daladala; hii ni gari ya serikali na wewe ni serikali, ni mali yako. Hivyo ndivyo ilivyo na kuna watu wanaoona bora mambo yabakie vivyohivyo. Hiyo ni hisani tunayofanyiana, tunapeana faraja kwa namna hiyo. Mfanya kazi wa serikali au wa taasisi ya umma huko Zanzibar, pale anapofiwa anaomba na anapatiwa gari ya serikali, dereva na petroli bila kulipia, ili iwachukue watu wake kwenda mazikoni na kuwarejesha. Gharama za mafuta na kuchakaa kwa

azanzibari tunalitumia sana neno Mhali au wengine Muhali. Huenda kwa vile tunafungamana sana, kivitendo, na maana ya neno hilo ambayo ni: jambo lilisowezekana au shida kulifanya kwa vile athari zake zitakuwa si nzuri, linaweza kuleta ugomvi, kutoelewana au bughudha baina ya watu (Kamusi ya Kiswahili sanifu ya TUKI). Umuhali umekuwa sasa sehemu ya utamaduni wetu. Badala ya kuwa mazoea mabaya tumeugeuza ati kuwa ni maadili bora ya kuigwa, ati ni kufanyiana hisani. Kuna hatari ya umuhali kuwa

gari inabeba serikali.

Nilijiuliza bima inakuwaje kwa abiria waliojazana pomoni ndani ya gari ya serikali pale, Mwenyezi Mungu aepushe, inatokea ajali? Sijapata jibu. Na kwa nini mterem- Hamna kanuni za kazi zinazotaja kwamba mkuu wa ko huo anaupata mtumishi

wa serikali au wa taasisi ya umma tu, na si raia mwengine? Hapo nahisi inakosekana haki. Niliambiwa hisani kama hiyo inawapa motisha wafanya kazi. Kweli?

UKURASA PAGE

18

UKURASA

19

ZANZIBAR Y O U R D A I M A H NEL IRN E O

LO G O

JAR IDA LA KILA MZAN ZIBARI


www.zanzibardaima.net Toleo 04 - 2013

WARAKA KUTOKA BONN

J AR I DA LA KILA MZA NZIBA RI


www.zanzibardaima.net Toleo 04 - 2013

ZANZIBAR D A I M A ONLINE

idara ya serikali anaweza kutoa nafuu na ureda huo kwa wafanya kazi wake. Bosi wa idara pamoja mchunguzi wa hesabu wote wanafumbia macho jambo hilo, wanataka waonekane wazuri mbele ya wenziwao. Umuhali. Mimi sipingi kufanyiana hisani na kupeana faraja wakati wa dhiki, hasa katika msiba. Ni utu, ubinadamu, lakini si kwa mgongo wa hazina ya pamoja ya serikali, tena kuwafariji kifedha pia watu ambao kwa vyovyote, kutokana na uluwa na uwezo wao wanazimudu kwa urahisi gharama za mazishi. Kama kufariji basi wafanya kazi wenzake wamsaidie mfiwa kwa kuchangia kutoka mifukoni mwao. Hili si suala la kutojali masaibu ya wenzako, lakini ni kwamba mwishowe sote, kama nchi, tunaharibikiwa. Nchi nyingi duniani hazifanyi Licha ya kuwa picha hii ya Ndagoni, Pemba, kuonyesha taswira ya umaskini lakini penye nidhamu ya ufuahivyo na pia mashirika ya taji mambo ipasavyo, kijiji kama hichi kinaweza kuwa alama ya utajiri wa watu na utamaduni wao. kimataifa yalioko hapohapo Zanzibar hayafanyi hivyo. Baada ya mazungumzo na Waziri wa Kijerumani hajarumani, Christian Wulff, Ni suala la uchumi, hasa mwenyeji wake ofisini, naye taka umuhali, alinisimulia alijiuzulu mwaka jana kutokwa nchi inayopata taabu Alizungumza kwa muda aliomba simu azungumze waziri wetu. Alifanya kazi kana na mbinyo wa umma kila mwaka kusawazisha wa dakika tano. Mjerumani na mkewe Tanzania. Alipayake kama inavyotakiwa. na uchunguzi uliofanywa bajeti yake. baadaye aliomba aambiwe tiwa simu na akazungumza Waziri huyo alimwambia na mwendesha mashtaka kiasi gani iligharimu kupiga mwenzake wa Tanzania: wa serikali akituhumiwa Waziri mmoja wa serikali ya ile simu ili alipe. Waziri wetu dakika 20. Dakika chache baadaye waziri wa KijeruNyinyi serikali zenu Afrika kwamba marafiki zake, Muungano, Mzanzibari, ali- akamwambia mwenzake ni maskini, lakini zinatumia wafanya biashara, wanipa hadithi kwamba waziri asifanye hivyo, yeye alikuwa mani akamuomba sekretari wake amletee waziri wetu kitajiri; sisi zetu ni tajiri, limpa mkopo wa kununua mwenzake wa kutoka Ujemgeni wake, na zaidi simu bili inayoonesha muda tunalazimika na tuko tayari nyumba na kugharamia rumani alimtembelea ofini ya serikali. aliozungumza na nambari kuishi kimaskini, inapohita- safari zake za likizo. Hayo sini kwake, Dar es Salaam. iliopigwa. Gharama ni mark jika. huenda, kisheria, yasioneBaada ya mazungumzo yao, Mwaka uliofuata waziri za Kijerumani 140. Ndugu kane kuwa ni uhalifu, lakini waziri wa Kijerumani aliom- wetu wa Kitanzania alifanya Aliyekuwa Rais wa Ujekwa Wajerumani yanatoa ba apatiwe simu ili azunziara ya kulipizia mjini Bonn. yangu waziri alilipa. gumze na mkewe Bonn.
UKURASA PAGE

harufu kwamba hisani hiyo aliofanyiwa rais hiyo huenda baadaye akailipia kwa kutumia cheo chake. Ni aibu na fedheha kwa mkuu wa nchi kufadhaliwa na kuikubali hisani kama hiyo akiwa madarakani. Novemba Mosi mwaka huu rais huyohuyo mstaafu atafikishwa mahakamani kwa mashtaka kwamba mwaka 2008 alilipiwa (mwenyewe anadai alikuwa hajui) na rafiki yake, mfanya biashara, gharama ya euro 719 kwa makazi katika hoteli na kula chakula. Takrima nayo pia, kwa Wajerumani, mara nyingi honekana ni hongo, rushwa, hasa inapomhusu mheshimiwa aliyomo serikalini. Hamna muhali hata kwa rais wa nchi. Nahisi uchapaji kazi katika utumishi wa serikali na mashirika ya umma uko chini kwa sababu ya umuhali wa maafisa kukubali mibinyo iliozoeleka kijamii, kutoa umbele kwa jamaa zao - mto wa shangazi na mjomba - japokuwa wako watu wengine wanaoweza kufanya kazi vizuri zaidi. Kuna ubadhirifu mkubwa wa mali za umma kutokana na umuhali.Tuwe majasiri wa kutumia maneno kama vile SINA, SITAKI, SIWEZI badala ya kudanganyana kwa maneno kama vile NITAJARIBU, NITAANGALI au NITAONA ambayo yanatufanya mwishowe tuwe watumwa wa umuhali.

20

UKURASA

21

ZANZIBAR Y O U R D A I M A H NEL IRN E O

LO G O

JAR IDA LA KILA MZAN ZIBARI


www.zanzibardaima.net Toleo 04 - 2013

Hatujawahi kuacha kusema


ya baadaye visiwani Zanzibar ulioacha kufanya uwezalo kupigania haki ya nchi hii japo kwa njia za kimya kimya zaidi. Katika awamu ya tatu na ya nne, kwa mfano, Serikali ya Zanzibar ilifanya juhudi za kusawazisha kasoro za Muungano (baadaye zimekuja kupewa jina la kero) kupitia vikao vya pamoja baina yake na Serikali ya Mungano.

MKEKA WA MWANA WA MWANA

J AR I DA LA KILA MZA NZIBA RI


www.zanzibardaima.net Toleo 04 - 2013

ZANZIBAR D A I M A ONLINE

Katika awamu ya tano, Serikali ilichukua hatua nyingi zaidi kuliko awamu yoyote kabla yake kuyashughulikia matatizo ya Muungano. Na Riziki Omar Ilifika hadi hata Rais wa awamu hiyo, Dk. Salmin Amour Juma, akiazima tuuheshimu mchango onekana kama mbogo aliyejeruhimkubwa sana wa viongozi wa machoni mwa uongozi wa Bara. wa Zanzibar waliopita kwa hatua ya Tume ya Mabadi- Salmin hakuwa akificha hisia zake liko ya Katiba inayoongozwa za kutoridhishwa na namna Muunna Jaji Mstaafu Joseph Warioba ya gano ulivyokuwa ukiendeshwa. kupendekeza muundo wa Muun- Msimamo wake ulikuwa wazi kagano wa Serikali Tatu. Iwapo hili tika kudai marekebisho kwenye ndilo hatimaye litakuwa chaguo la maeneo kadhaa, hasa masuala wananchi kwenye kura ya maoni ya uchumi, orodha ya mambo ya ama la, ukweli utabaki kwamba Muungano na suala la Jumuiya ya Wazanzibari kwa mara nyengine Afrika Mashariki. tena walipuliza zumari na walio Awamu ya sita nayo pia inajulikana Mrima wakaicheza. wazi kwa msimamo wake juu ya Ukimwacha Mzee Aboud Jumbe suala la nishati ya mafuta na utamMwinyi, ambaye alilazimishwa ku- bulisho wa nchi ya Zanzibar ndani jiuzulu nyadhifa zake zote serikalini ya Jamhuri ya Muungano. Mara tu na chamani na mkutano mkuu wa baada ya Rais Amani Karume kuChama cha Mapinduzi (CCM) chini ingia madarakani, aliunda kamati ya uwenyekiti wa Mwalimu Julius ya wataalamu ambayo ilichambua Nyerere, kwa sababu tu ya kuite- kasoro za Muungano na kupendetea Zanzibar ndani ya Muungano, keza mambo ya kupunguzwa au hakuna utawala wa awamu yoyote kuongezwa pamoja na utaratibu

Rais wa Awamu ya Sita wa Zanzibar, Amani Karume, ambaye serikali yake ilipendekeza kuwa na mabunge mawili ya Muungano. wa kuendesha masuala ya Muungano tu na lenye uwakilishi sawa baina ya kisera, kiutawala na katika kutunga Tanganyika na Zanzibar. sheria za Muungano huo. Kwa hivyo, kama mtu anafuatilia ukPendekezo moja mahsusi la kamati weli, atakuta mambo mawili: kwanza, hiyo na ambalo linaonekana kuakisi- Wazanzibari na viongozi wao ndio ka kwenye Rasimu ya Katiba Mpya waliojenga taswira ya mabadiliko ya ni lile la Bunge la Tanzania kuwa na Katiba yajayo kwa kuwa, na hili ndilo mabaraza mawili, yaani Baraza la la pili, hawakuwahi kukaa kimya paChini (Lower House) la kushughulikia napohusika hatima ya nchi yao ndani mambo ya Tanganyika tu na ambamo ya Muungano. Zanzibar haitokuwa na wajumbe na Baraza la Juu (Upper House) ambalo Hili ni jawabu kwa wale wanaouliza litashughulikia mambo ya Muungano walikuwa wapi Wazanzibari siku zote hizo wanapodai nchi yao imekuwa ikichukuliwa dhiraa kwa dhiraa bila ya ridhaa yao na ikawa leo ndo wanalalamika. Jawabu ni kwamba kwa muda wa takriban miaka 50 ya Muungano, siasa za Serikali ya Muungano juu ya Zanzibar zimewanyima Wazanzibari fursa ya kuziondosha kero za Muungano. Ndio maana leo hii wengine tunashangaa kuwaona viongozi wa CCM wa Zanzibar, kuwa hata baada ya mihanga yote ambayo Wazanzibari waUKURASA

UKURASA PAGE

22

23

ZANZIBAR Y O U R D A I M A H NEL IRN E O

LO G O

JAR IDA LA KILA MZAN ZIBARI


www.zanzibardaima.net Toleo 04 - 2013

MKEKA WA MWANA WA MWANA

J AR I DA LA KILA MZA NZIBA RI


www.zanzibardaima.net Toleo 04 - 2013

ZANZIBAR D A I M A ONLINE

meitoa, bado wanathubutu kungangania kile kile ambacho serikali yao, katika awamu mbalimbali, imekikataa. Ni vipi leo viongozi wa CCM ya Kisiwandui wakawa wanapingana na ukweli kwamba hawajawahi kusikilizwa hata siku moja juu ya namna Muungano huu unavyopaswa kuendeshwa na wanangangania kuyapinga mapendekezo ya Rasimu ya Katiba, kwa kuwa tu wanadhani yatahatarisha kuwepo kwao madarakani? Hawasomi, hawajifunzi jitihada ambazo Zanzibar ilijaribu kuzichukua huko nyuma lakini ikaangukia kwa pua na kwamba sasa umefika wakati wa kulimaliza jambo hili dumu daima? Kwa mfano, baina ya mwaka 1990 na 2003, Serikali ya Zanzibar peke yake ilishaunda kamati 12 za kutatua kero za Muungano: Kamati ya Baraza la Mapinduzi (Kamati ya Amina) ya 1992, Kamati ya Rais ya Kupambana na Kasoro za Muungano (Kamati ya Shamhuna) ya 1997, Kamati ya Rais ya Kuchambua Ripoti ya Jaji Kisanga (Kamati ya Salim Juma Othman), Kamati ya Kuandaa Mapendekezo ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Juu ya Kero za Muungano (Kamati ya Ramia) ya 2000, Kamati ya Baraza la Mapinduzi Juu ya Sera ya Mambo ya Nje, Kamati ya Rais ya Wataalamu Juu ya Kero za Muungano ya 2001, Kamati ya Baraza la Mapinduzi ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, Kamati ya Mafuta, Kamati ya Madeni Baina ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya MuunUKURASA PAGE

Rais wa Awamu ya Tano ya Zanzibar, Dk. Salmin Amour, ambaye naye alikuwa akichukuliwa na Bara kama kiongozi asiyesemezeka lilipohusika suala la nafasi ya Zanzibar kwenye Muungano. gano wa Tanzania, Kamati ya Suala la Exclusive Economic Zone (EEZ), Kamati ya Masuala ya Fedha na Benki Kuu na Kamati ya Rais ya Masuala ya Simu (1996 1999). Mbali na kamati hizo, SMZ na SMT zilishafanya vikao vya pamoja visivyopungua 80 katika ngazi mbali mbali, ili kuzungumzia kero za Muungano. Vile vile serikali hizo mbili mwaka 1994 ziliomba msaada wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) ili kuzishauri kuhusiana na Benki Kuu, mgawano wa misaada na uhusiano wa kifedha. Licha ya kamati na vikao vyote hivyo, Muungano huu umeendelea kukabiliwa na matatizo yale yale yaliyoundiwa kamati na au yaliyowekewa vikao. Kero zilizozungumziwa mwaka 1984 katika vikao vya pamoja ndizo hizo hizo zilizozungumzwa katika ripoti ya Shelukindo ya 1992 na katika mwafaka baina ya SMT na SMZ wa mwaka 1994 na kuzungumzwa tena katika kamati ya wataalamu ya SMZ ya 2001. Jibu ni kuwa, Muungano huu una kasoro za kimaumbile na za kuzaliwa nazo. Unakosa uwiano na uadilifu baina ya pande mbili zinazouunda. Umetawaliwa na sahau au dharau kwamba Tanganyika na Zanzibar zina mamlaka sawa kwenye Muungano huu na sio kwamba upande mmoja una nguvu zaidi kuliko mwengine.

Wakuu wa CCM/Kisiwandui wanaopingana na matakwa mapana ya Wazanzibari, wa- Basi hata hili hawalioni? Wakiliona hawalinapaswa kujiuliza ni kwa nini juhudi zote semi? Walionao wakalisema, wanawafukuhizo zimeshindwa? za na kuwatungia majina mabaya mabaya. Tuwaeleweje wenzetu hawa?

24

UKURASA

25

ZANZIBAR Y O U R D A I M A H NEL IRN E O

LO G O

JAR IDA LA KILA MZAN ZIBARI


www.zanzibardaima.net Toleo 04 - 2013

Hii ndio tindikali ipaswayo kupigwa vita

MAKALA MAALUM
ghulikia mgonjwa kwa mujibu wa kiwango, aina ya tindikali iliyotumika na pia urefu wa muda baina ya pale mwathirika aliposhambuliwa na kuwa amepata huduma ya mwanzo ya kuoshwa kwa maji au tindikali hiyo kuyeyushwa kwa viyeyushaji vyake. Mtaalamu mmoja wa kemia ameiambia Zanzibar Daima Online kwamba baadhi ya tindikali kama vile salfuriki ni sawa na moto ulioko kwenye hali ya kimiminika, kwa hivyo mtu anapomwagiwa ni kama aliyemwagiwa moto mwilini mwake. Kwa haraka sana, tindikali huweza kuila ngozi, sehemu ya mafuta kwenye ngozi hiyo na katika baadhi ya matukio, huweza kuzama hadi kwenye mifupa. Nyusi na midomo inaweza kuharibiwa kabisa na pua na masikio kuathirika vibaya. Kwa mujibu wa mtandao wa Wikipedia, tafiti zimeonesha kuwa madhara yafuatayo yamewahi kuwakumba walengwa wa mashambulizi haya: Fuvu la kichwa kuharibiwa na nywele kupotea kabisa Mkano wa sikio kuharibiwa na kusababisha uziwi Kope huungua kabisa na kuyawacha macho yakiwa wazi na makavu na hivyo kupelekea upofu Mkano wa pua kuharibiwa na hivyo pua yenyewe kuondoka kabisa Mdomo kutanuka na kusinyaa na kuyaweka meno nje na hivyo kusababisha ugumu wa kuzungumza na kula Kuharibiwa kwa mfumo wa kuingia na kutoa hewa mwilini kwani viungo kama pua na mdomo ambavyo vinahusika huwa vimeathirika. Hayo ni matokeo ya mashambulizi ya tindikali kimwili, lakini kama tulivyosema matatizo zaidi huwa kisaikolojia, kwani utafiti unaonyesha kuwa waathirika wengi wa mashambulizi haya hukabiliwa na maradhi ya mfadhaiko, wasiwasi na wengine hata hupoteza akili zao moja kwa moja, kwani taswira ya maumbile yao mapya huwa inawaandama kama jinamizi. Katika hili, huhitajika msaada wa ziada kutoka kwa familia, marafiki na jamii kwa ujumla ili kumuonyesha mwathirika wa mashambulizi

J AR I DA LA KILA MZA NZIBA RI


www.zanzibardaima.net Toleo 04 - 2013

ZANZIBAR D A I M A ONLINE

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete, akimjuulia hali Sheikh Fadhil Soraga katika Hospitali ya Muhimbini mwishoni mwa mwaka jana
This is caption text for this

Na Mwandishi Maalum
wabaya wanaozitumia dhidi ya wenzao kwa njia za kikatili kama ambavyo imekuwa ikishuhudiwa. Kwa mujibu wa watafiti, nchi ambazo zimeathiriwa sana na mashambulizi haya ni pamoja na Bangladesh, India, Pakistan, Cambodia, Vietnam, Laos, Hong Kong, China, Uingereza, Kenya, Afrika ya Kusini, Uganda, Afghanistan, Iran na Ethiopia. Hata hivyo, ni nadra kwa waathirika wa mashambulizi haya kupoteza maisha kwa sababu ya mashambulizi yenyewe. Kwa mujibu wa Wakfu wa Wahanga wa Tindikali ya Pakistan, idadi kubwa ya walengwa hao huendelea kuishi muda mrefu baada ya kushambuliwa. Lakini ukweli ni kuwa wanakabiliwa na changamoto za kimwili zinazohitaji operesheni nyingi na za muda mrefu na pia za kisaikolojia ambazo nazo zinahitaji msaada mkubwa wa ushauri kutoka kwa watu wa karibu na jamii kwa ujumla katika kila hatua ya kupona kwao kimwili. Kwa upande wa matibabu, madaktari humshu-

ashambulizi ya tindikali yanafasiriwa kama kitendo cha kurusha tindikali au kemikali yoyote inayofanana nayo kwenye mwili wa mtu kwa lengo la kuuharibu mwili huo, kumtesa au kumuua mtu huyo. Kwa fasili yake, itafahamika wazi kwamba mashambulizi haya ni uhalifu mkubwa na wanaoufanya ni wahalifu wasiovumilika. Mara nyingi wahalifu hawa huwarushia walengwa wao tindikali usoni, wakaunguza na kuziharibu ngozi na baadhi ya wakati maji hayo ya kemikali huzama hadi kwenye ngozi. Tindikali maarufu zinazotumika ni pamoja na salfuriki, naitriki na haidrokloriki, ambazo visiwani Zanzibar kama ilivyo kwengineko duniani zinapatikana kirahisi zikiwa katika miundo tafauti. Huwa kama maji kwenye betri za magari, kemikali kwenye viwanda vya kienyeji vya sabuni na vipodozi majumbani au hifadhi ya madawa kwenye maabara. Kwa hivyo, ni sahihi kusema Zanzibar inaishi ndani ya duara la silaha hizi za kemikali, ambazo ni rahisi kuangukia mikononi mwa watu

haya kwamba maisha yanaweza kuwa mazuri tena hata kama mwili au sehemu ya mwili huo imepata ulemavu wa kudumu. Mashambulizi kama haya mara nyingi huwafanya walioathirika kubakia kuwa wategemezi wa familia zao kwa muda wote uliobakia wa maisha yao. Inapotokea kwamba wao walikuwa ndio wanaoihudumia familia hiyo, basi hilo huiingiza familia nzima kwenye uathirika. Kazi nyengine ambazo waathirika walikuwa wakizifanya kabla ya kushambuliwa zilikuwa zikitegemea sura zao, na inapotokea kwamba hawawezi tena kurudi kwenye kazi hizo, lazima kuwe na mpango maalum wa kijamii na kitaifa kuwarudishia maisha yao ya kawaida. Katika baadhi ya mikasa hii, familia zimeporomoka au kuvunjika kabisa. Kwa mfano nchini Uganda asilimia 25 ya waume wenye wake walioathiriwa, waliwaacha wake zao, ingawa ni asilimia 3 tu ya wanawake waliowakimbia waume zao waliomwagiwa tindikali. Na kwengineko, wahanga wa mashambulizi haya ambao hawajaoa au kuolewa, wamejikuta wakipoteza kabisa matumaini ya kuanzisha familia zao wenyewe, maana ni shida kuwapata wenza wanaowakubali kama walivyo wakiwa na miili iliyoharibiwa. Tafiti zimeonyesha kwamba kuna njia kadhaa za kukabiliana na mashambulizi haya hatari na ya kikatili duniani. Nchi kama Bangladesh, ambako mashambulizi haya yamekuwa yakipungua, mafanikio yake yametokana na marekebisho makubwa kwenye mifumo ya kisheria. Hata hivyo, haja kubwa pia ipo kwenye uanzishwaji wa taasisi zisizo za serikali katika kujenga uwelewa wa umma kwa tatizo hili na pia kuwasaidia walioathirika kurudi kwenye maisha ya kawaida. Kama ulivyo uhalifu mwengine wowote, huwa hasa umetayarishwa na jamii husika, wahalifu wakabakia na kazi ya kuutekeleza tu. Mashambulizi ya tindikali pia yanaingia kwenye kundi hilo. Jamii isiyo na mwamko wa kutosha kuhusu tindikali huwa inajitayarishia yenyewe uhalifu wa kemikali hizo. Hili ndilo linalofanya pawe na hoja na haja ya kuwa vuguvugu la wananchi kupingana na mashambulizi haya ya kinyama.
UKURASA

UKURASA PAGE

26

27

ZANZIBAR Y O U R D A I M A H NEL IRN E O

LO G O

JAR IDA LA KILA MZAN ZIBARI


www.zanzibardaima.net Toleo 04 - 2013

BARZA YA JUMBA MARO

J AR I DA LA KILA MZA NZIBA RI


www.zanzibardaima.net Toleo 04 - 2013

ZANZIBAR D A I M A ONLINE

Wimbo mbaya wa magazeti ya Bara


kimataifa, au yameandikwa baada ya uchunguzi wa waandishi wao. Lakini kwa fikra zangu wahariri wanapaswa kuwa na nadhari kuwa makala yatokayo nje yanayoeleza kuwa kuna mvutano na uhasama wa kidini na wenye mnaso wa KiAlqaida au wa Ki-Al-Shabaab, hayawezi kutumiwa tu hivi hivi. Kwa itakavyokuwa na kwa kipimo chochote kile Mhariri wa gazeti lolote lile la Bara anapaswa kuwa anaijua Zanzibar. Mbali na hayo alipaswa pia kufanya juhudi kuyatia makala hayo katika mizania na kwa hivyo yawe yametumika pia kwa faida ya Zanzibar, ambayo ni sehemu ya taifa hili.

Na Ally Saleh

aswahili tunajua sote msemo maarufu wa Wimbo Mbaya Hachombezewi Mtoto. Kwa mila na utamaduni wetu mzazi atajiepusha kwa kila hali kuimba wimbo aina hiyo ambao unaweza kumpeleka au kumuelekeza mtoto pabaya.

Upotoshaji mkubwa uliofanywa katika makala kama hayo, au hata maoni ya Wahariri yasiojenga, unaidhalilisha Zanzibar. Lakini upoLakini hii haiwazui watu toshwaji mkubwa ni ule wa wengine wasimwimbie wim- Mhariri kukubali makala hayo bo mbaya mtoto wako. Na yachapishwe katika gazeti miongoni mwa watu wengine lake akijua kuwa yanauni pamoja na ndugu zako kashifu upande mmoja wa kama ilivyotokea hivi karibuni Jamhuri ya Muungano, yaani kwa magazeti ya Tanzania Zanzibar. Bara kuchapisha makala yenye kuiimbia nyimbo mbaya Kwa kuyakubali makala hayo sana Zanzibar. Mhariri anakuwa anakubali kuwa hali iko mbaya sana Kisingizio chao cha kuchapiZanzibar kwa sababu ya sha ni kuwa makala hayo matukio ya watu kumwagiwa yamepatikana kutoka kwe- tindikali na kwa sababu za nye mashirika ya habari ya kidini wakati waliotiwa tindiUKURASA PAGE

Kamishna wa polisi Zanzibar Mussa Ali Mussa


kali ni pamoja na Waislamu akiwemo Sheikh Fadhil Soraga. Na wakati Tanzania Bara nako tindikali inatumika, na ambako pia risasi, mabomu sio vitu vigeni, tena vyereje kwa Zanzibar iwe mwao? Kama hisia za kuwepo kwa mtafaruku wa kidini ni kwa sababu ya kupata nguvu Uamsho, Mhariri wa gazeti anapaswa kujua kuwa jumuiya ya Uamsho imepata nguvu si kwa ajili ya mtizamo wa kidini ila ni kwa sababu ya kudai haki za Wazanzibari. Na mchakato wa Katiba kwa kuhaya Bara si mageni pia. dai Zanzibar ipate haki zake kamili ndani ya Jamhuri ya Mhariri anajua hilo kwa saMuungano. Kamwe Uamsho babu Uamsho imesajiliwa, haijasema kuwa inataka Zanimefanya kazi nyingi za kizibar ijitenge wala Zanzibar jamii lakini jina lake limeingia iwe dola ya Kiislamu. dosari katika kipindi hiki cha
UKURASA

28

29

ZANZIBAR Y O U R D A I M A H NEL IRN E O

LO G O

JAR IDA LA KILA MZAN ZIBARI


www.zanzibardaima.net Toleo 04 - 2013

BARZA YA JUMBA MARO

J AR I DA LA KILA MZA NZIBA RI


www.zanzibardaima.net Toleo 04 - 2013

ZANZIBAR D A I M A ONLINE

UJUMBE KWA KAMISHNA MUSSA


Kinachonisikitisha zaidi ni kuona Serikali ya Zanzibar imekaa kimya, burdan wa sururi, haya yakifanyika na yakifanywa na ndugu zao wa damu. Haiwezekani wala haikhalis kabisa kwa Serikali ya Zanzibar kulinyamazia suala kama hili. Naamini ingekuwa jambo hilo limefanywa na gazeti la Zanzibar Leo kuchapisha makala yanayoipaka matope Serikali ya Muungano basi Serikali hiyo ingekuwa imeshafanya vishindo dhidi ya Zanzibar. Kama ningepewa fursa ya kuishauri Serikali ya Zanzibar katika hili, basi inatosha kuwaambia kuwa wawasiliane moja kwa moja na wenzao wa Tanzania Bara juu ya hujma hii. Lakini wakati nyimbo mbaya ikiimbwa upande wa pili wa bahari, hata humu ndani pia mwenzetu mmoja, Kamishna Mussa Ali Mussa, naye amechukua tarumbeta akipaza nyimbo kama hiyo, anapiga zumari ndani ya nyumba yake. Katika kipindi hiki cha mtikisiko wa mashambulizi ya tindikali, ambayo wengi tunayalaani kwa nguvu zote kuwa ni ya kinyama na yasiovumilika, Kamishna Mussa ametoka hadharani mnasaba na hilo akisema kuwa kuna wapiganaji wa Al-Shabaab waliokamatwa wanaotaka kwenda kupigana Somalia.

Nataraji uungwana wa Kamishna Mussa, pamoja na cheo chake ni muhimu kwa maslahi ya Zanzibar, maana nchi itaendelea kuwepo na kwa vyovyote vile Uislamu hapa kwetu hautaweza kufutika, ila Uislamu wa siasa kali hatuutaki wala hatuukaribishi, na tusitoe dhana kwa wengine kuwa una nafasi.

kulenga Wakristo. Al-Shabab hutumia silaha, tena za maangamizi, tena hulenga maeneo ya kistratajia na zaidi hukusudia kutia hasara kubwa ya mali au maisha. Pili, nyimbo hiyo mbaya ya Kamishna Mussa ina mwangi mkubwa. Je, alitaka kusema kuna vikundi vya siri (cells) vya Al-Shabab hapa Zanzibar na kama vipo waliopatikana ni wachache tu kati yao, na kama wapo wengine kwa nini akatoa taarifa hizo hadharani wakati bado hawajatiwa mbaroni? Ingawa kuna Wazanzibari waliowahi kuhusika na matukio ya kigaidi, hatujawahi kusikia bado kama kuna vikundi vyovyote vya siri humu ndani, na kutangaza kama Al-Shabaab wamepita tu, maana yake ni kuiogopesha na kuipelekea Zanzibar itengwe bilashi. Inafaa na ni muhimu matamshi ya Kamishna Mussa yafafanuliwe na yaelezewe katika usuli mwema la sivyo yanaweza kuwa na hasara kubwa kwa Zanzibar, kwa sisi wenyewe kujiimbia nyimbo mbaya kuwa kumbe Al-Shabaab wameweza kufika Zanzibar. Ugumu bila ya shaka utakuja tunapotaka kujipapatua kwa sababu ya kauli ambayo pengine ilipaswa kuzuiwa au kufanyiwa utafiti zaidi. Katika mazingira kama hayo humkumbuka mjomba yangu Faisal Mbamba aliyewahi kuniusia, Bora kujikwaa dole utatia chokaa, kuliko kujikwaa ulimi. Nataraji uungwana wa Kamishna Mussa, pamoja na cheo chake ni muhimu kwa maslahi ya Zanzibar, maana nchi itaendelea kuwepo na kwa vyovyote vile Uislamu hapa kwetu hautaweza kufutika, ila Uislamu wa siasa kali hatuutaki wala hatuukaribishi, na tusitoe dhana kwa wengine kuwa una nafasi.
UKURASA

Hili ni suala zito.


Sijui kama Kamishna Mussa alitaka kuyaunganisha mashambulizi hayo ya tindikali na kundi hilo, lakini mantiki ya kawaida imekataa kwa sababu mashambulizi hayo hayana mwelekeo wa ki Al-Shabab kwa aina ya silaha na pia kulenga mtu mmoja mmoja, na zaidi pia
UKURASA PAGE

30

31

ZANZIBAR Y O U R D A I M A H NEL IRN E O

LO G O

JAR IDA LA KILA MZAN ZIBARI


www.zanzibardaima.net Toleo 04 - 2013

KALAMUYA BIN RAJAB

J AR I DA LA KILA MZA NZIBA RI


www.zanzibardaima.net Toleo 04 - 2013

ZANZIBAR D A I M A ONLINE

Jinsi wanasiasa wetu wanavyotuziba midomo


Na Ahmed Rajab

anasiasa ni wanasiasa. Na wa kwetu si tafauti sana na wa kwengine. Wana khulka moja, sifa moja na tabia moja. Aghalabu huukimbia ukweli.

Mbinu hiyo ni moja ya silaha za wanasiasa. Na ni silaha Labda wanavyofikiri ni kuwa za hatari. kazi yao ni ya kuuchekesha Wanasiasa hutuziba miumma na kwamba kila domo yetu, hutufanya tunwakiwatukana mahasimu yamaze, pale wanapoanza Lau wangaliweza kuzao, na mara nyingine hata kutoa shtuma za kibinafsi kaa pamoja wakajadiliwenzao, sisi hufurahi. dhidi ya wanasiasa mahaana mambo kiungwana. Kwa nini wasifikiri hivyo simu zao. Wakaujadili ukweli. Lakini ikiwa sisi wenyewe tutumekwishazoea kuwaona Tuchukue mfano wa wawakizozana, wakitukanana. nawapigia makofi na wanasiasa fulani wa Chama nawake wanawapigia Wakiukimbia ukweli. cha Mapinduzi (CCM) wavigelegele? naposimama jukwaani na Wengine huwatukana wenHalafu kuna zile nguvu kuwashtumu Wazanzibari zao kwa kistaarabu. Wenmaalum wanazohisi kuwa wenye kutaka muundo wa gine huwa hawana adabu. wanazipata wanapokuwa Muungano ubadilike uwe Lakini wote wamezoea wamesimama juu ya majukwa Mkataba au wa Serikali kutukana. Ndio maana kuna waa wakipayuka mbele ya Tatu kuwa wana lengo la wengi miongoni mwetu vipaza sauti. kuuvunja Muungano. Au tunaoziona siasa kuwa ni kuwa wanataka kuurejesha chafu. Hapo ndipo wanapokoroga usultani. mambo. Hapo ndipo waNa wapo wanasiasa ambao napokuwa wevi. Huyaiba Japokuwa hao wanasiasa kwa vitendo vyao na kauli maneno kwa kuyatumia wa CCM wanatambua wezao hujifanya wenyewe vibaya. Wanapotosha nyewe kwamba wayaswawe wachafu. maana ya maneno; wanay- emayo si ya kweli, wanaSina azma ya kutaja majina. apinda maana na kuyafanya chodhamiria khasa kufanya Nikifanya hivyo nitawapa maneno si tu yasiwe na ni kuwachimba wale wenye umuhimu wasioustahili hao maana yake asilia bali hata kutetea muundo wa Muunwahuni wa kisiasa. Sote hufika hadi ya kuyafanya gano ugeuzwe na Zanzibar tunawajuwa. Na wao wemaneno yasiwe na maana iwe na mamlaka yake kanyewe wanajijuwa. Wayoyote. mili. Wanataka watu wanazipa siasa jina baya. Hilo siwaamini tena hao wenye Sisi tunaowasikiliza huwa pengine hawalijui. kuipigania Zanzibar. hatuna la kufanya ila kuduPengine makosa si yao waa. Hiyo ni moja ya hila Kwa hakika, tukichunguza peke yao; pengine sisi pia zao. Ni moja kati ya mikakwa makini tutaona kwamni wakosa. Ni wakosa kwa kati yao ya kutufanya tuzibe ba hotuba za wanasiasa sababu hao wanasiasa wetu midomo yetu, tunyamaze, zina malengo kadha wa pengine wanaamini kwam- kwani huwa hatujui tuseme kadha; na kati ya hayo lengo

ba tunachokitaraji kutoka kwao ni kuyasikia matusi yao.

nini.

Wafuasi wa Chama cha Mapinduzi wakishagiria moja ya hotuba ya viongozi wao. moja tu lilitakiwa liwe ni la kusema ukweli. kuyatumia maneno fulani na kuyafanya kuwa kama yake yenyewe kana Juu ya yote hayo kwa kwamba vile vyama vingine kawaida sisi tusio wanahavina uhalali wa kuyatumia siasa huwatarajia viongozi maneno hayo. Kuna mifano wetu wa kisiasa wawe waa- mingi ya maneno hayo lakini minifu, waadilifu na wenye yanayonijia haraka kichwani kusema kweli. ni uzalendo , mapinduzi, maadui wa nchi, wapinga Kwa kuwaziba mdomo wa- maendeleo na wenye nchi. nanchi wanasiasa wanakuwa wanawapokonya uwezo Namna maneno hayo yanawao wa kusema, wa kuhoji vyotumiwa na chama hicho na wa kujizatiti. Wanawani aina ya propaganda na fanya wasiweze kusema. daima katika siasa tunaona jinsi propaganda inavyobKuna njia nyingine wanayo- adili thamani ya maneno na tumia wanasiasa kuwankushusha hadhi yao. yamazisha watu. Huwanyamazisha kwa kuwanyima Nchini mwetu ambapo msamiati wa kueleza madai vyombo vya habari vya yao. serikali vinatoa propaganda ni rahisi kuona jinsi kutoaHebu tuchukue tena mfano miniana na uwongo ulivyowa CCM/Zanzibar. Washamiri. Kwa hivyo, hata nasiasa wake wamezoea ikiwa watu wa jamii fulani wanaweza kupokea habari za kuaminika, kwa kupitia kwa mfano, mtandao wa intaneti, hao watu daima huwa hawaziamini. Kuwaziba midomo wananchi ni aina moja ya propaganda. Kwa hivyo, katika kuwanyamazisha watu, kuwafanya wasiweze kusema, wanyamaze tu, wanasiasa wanakuwa wanamwomdoshea mtu au kundi la watu uwezo wa kuwasiliana na wengine. Lakini nafikiri kwamba kwa mazingira yetu ya kisiasa yalivyo siku hizi Zanzibar ambapo tuna shauku kubwa ya kuuimarisha Umoja na Mshikamano wetu ni muhimu tuzingatie hatari za kuitumia vibaya lugha na hatari za kuipotosha kwa faida ya wanasiasa wenye kuyafikiria maslahi yao tu.
UKURASA

UKURASA PAGE

32

33

ZANZIBAR Y O U R D A I M A H NEL IRN E O

LO G O

JAR IDA LA KILA MZAN ZIBARI


www.zanzibardaima.net Toleo 04 - 2013

KAULI YA MWINYI MKUU

J AR I DA LA KILA MZA NZIBA RI


www.zanzibardaima.net Toleo 04 - 2013

ZANZIBAR D A I M A ONLINE

Kamishna Mussa hakufikiri ili atende

Na Jabir Idrissa

wamejeruhiwa kwa risasi. Mtu kwa hisia tu kwamba labda fulani anahusika na ubaya huu au ule, kama ni ubaya kweli, anapigwa risasi. Kwa hulka yangu, sipendi udhalimu, nachukia utawala wa kibabe, napinga unyanyasaji na udhalilishaji binadamu kwa namna yoyote ile. Inapotokea hayo nisiyoyapenda, yale ninayoyachukia na ninayoyapinga, yanatendwa juu ya watu dhalili kihali na wale wanaohitaji msaada sana ili kuondokana na udhalilifu huo na kuwa wanaopata matumaini badala yake, nakuwa nachomwa zaidi. Sasa kwa kuwa sipendi sera za mabavu, maonevu na udhalilishaji binadamu hasa wanyonge, na kwa kujua kwamba Marekani ni taifa mshiriki mkuu wa matendo hayo mabaya kutokana na kampeni inazoziendesha kwa visingizio vya kupamMoja ya kifungu katika sheria-shinikizo za kupambana na ugaidi zilizoandikwa Marekani na kuenezwa mabara yote duniani kwa ushawishi wao, ni kile kinachoruhusu mtu kuwekwa kizuizini wenyewe wanaita kitendo hiki kwa jina zuri la kumhifadhi. Eti mtu anahifadhiwa asikochagua kwa namna yoyote ile kwa muda usiojulikana. Ndio maana wengine tuliamini mapema kwamba katika kampeni ya kupambana na ugaidi iliyoanzishwa na Marekani baada ya mashambulio mawili ndani ya nchi yake, mwaka 2001 Makao Makuu ya Wizara ya Ulinzi (Pentagon), Washington, na Kituo cha Kimataifa cha Biashara (WTC), New York, ilikuwa ni kueneza chuki UKURASA

ama kuna jambo ambalo nililichukia tokea siku ya kwanza tu lilipotajwa kuhusiana na mpango wa kudhibiti ugaidi duniani, basi ilikuwa ni uamuzi wa Marekani kushinikiza mataifa ya dunia kutunga sheria inayohusu kampeni yake ya kupambana na ugaidi. Hili jambo lilinikera kwa kiwango kikubwa. Sababu ni moja tu: huwa sipendi amri za Marekani kwa mataifa maskini kama haya yetu ya barani Afrika. Siku zote nimekuwa nikiamini kuwa amri za taifa hili lenye nguvu kubwa za kiuchumi na kijeshi, kwa nchi zetu, huwa hazizingatii maslahi ya kweli ya nchi zetu.

bana na ugaidi katika nchi mbalimbali, nilikerwa niliposikia Marekani inashinikiza mataifa mengine kutunga sheria ya ugaidi. Nilijua ukumbatiaji wa shinikizo lile utaleta madhara makubwa kwa nchi zetu na watu wake. Kwanza kwa taifa tu kutunga sheria inayotokana na inayofuata misingi iliyoshawishiwa na taifa lenye nguvu, peke yake ni sawa na taifa hilo kukubali utumwa. Si uongo, sheria nyingi zilizotungwa na nchi za

Kiafrika, achilia mbali za mabara ya Asia na Amerika ya Kusini, zimezusha malalamiko mengi. Zilitungwa kwa njia ya zimamoto, kwa hivyo hazikuwa bayana; zilikosa utashi wa kukubalika na kwa kweli, zililalamikiwa na kupingwa. Hali hiyo inaweza kutafsirika kuwa na maana ifuatayo: sheria zilizoshinikizwa kwetu, zimeleta matatizo katika nchi zetu. Ina maana sheria hizi hazikutuletea tija iliyokusudiwa bali zaidi, zimejenga nguvu kwa utawala kukandamiza watu wake.

Watu katika nchi ambako sheria-shinikizo zilitungwa wameumizwa na wangali wanaendelea kuumizwa. Utasikia mtu kavamiwa nyumbani kwake, kapekuliwa, akutwe au asikutwe na kilichokuwa kinatafutwa katika upekuzi, anawekwa kizuizini. Haelezwi hayo yanafanywa kwa sababu gani. Wala mtu huyo haelezwi kama kuna tuhuma anazokabiliwa nazo ili atumie haki yake ya kujitetea. Katika kutumikia sheria-shinikizo, wapo watu waliouliwa kwa kupigwa risasi. Wapo wengi

UKURASA PAGE

34

35

ZANZIBAR Y O U R D A I M A H NEL IRN E O

LO G O

JAR IDA LA KILA MZAN ZIBARI


www.zanzibardaima.net Toleo 04 - 2013

KAULI YA MWINYI MKUU

J AR I DA LA KILA MZA NZIBA RI


www.zanzibardaima.net Toleo 04 - 2013

ZANZIBAR D A I M A ONLINE

dhidi yao wenyewe duniani kote. Uenezaji wa chuki umetokea kwa sababu kwa wale wanaoumizwa na kampeni hiyo, kupitia zile sheria-shinikizo, wanachokiona si kingine isipokuwa kunyanyaswa na kudhalilishwa na wasimamiaji wa sheria ya ugaidi. Na kwa sababu wanaoumizwa kwa kunyanyaswa na kudhalilishwa pamoja na kujeruhiwa na au kuuliwa, wanajua kuwa yote hayo yanatokana na shinikizo za Marekani. Kwa hivyo walimwengu wanajua kwa sababu ya shida za Marekani, wao wanaumizwa. Sasa, inasikitisha kukuta Zanzibar ina mtendaji wa taasisi muhimu ya dola anayejifakharisha kwa kutamka kuwa wamekamata watu wanaoshirikiana na makundi ya Al Qaeda na Al-Shabaab. Inaonekana Kamishna wa Polisi Zanzibar, Mussa Ali Mussa, hata haelewi madhara ya kutoa matamshi kama hayo. Ni bahati mbaya sana kuwa ofisa wa ngazi ya juu katika Jeshi la Polisi kama yeye, haelewi madhara ya alichokifanya mwanzoni mwa wiki hii alipokutana na waandishi wa habari kuzungumzia uchunguzi wa tukio la kumwagiwa tindikali Padri Joseph Anselmo Mwangamba. Hivi ni kweli hajui kuwa kutamka hivyo ni kushawishi Marekani na washirika wake waamini kuwa Zanzibar inafuga watenda ugaidi? Hajui kuwa ukishatajwa unafuga

watenda ugaidi nchini kwako unakaribisha maaskari wa mataifa hayo kuja kuchunguza? Hajui yote haya? Ndiyo nikasema ni bahati mbaya sana kama hajui. Uchunguzi wa kuangalia kama kweli Zanzibar inafuga au kuhifadhi watenda ugaidi, kwa kufahamu au kwa kutofahamu, hufanywa na matokeo yake mara nyingi ni kuigharimu nchi na watu wake. Labda Kamishna Mussa hafuatilii yale yanayotokea kwenye nchi zinazotajwa kwa hilo. Dunia inashuhudia namna nchi zinazotajwa kutumika kwa ajili ya kuhifadhi watenda ugaidi zinavyokumbwa na matatizo ya kiusalama kila siku. Ikipita wiki bila ya kutokea tatizo hakika mnamshukuru Mola aliyewaumba. Ni shughuli pevu.

polisi na Serikali kwa jumla. Ni nani walioingilia mikutano ya Jumuiya ya Uamsho na kuiletea nchi fadhaa kubwa mbele ya macho ya kimataifa? Ni nani waliofanikisha mpango wa kuwanyamazisha masheikh kwa kuwakamata na kuwatia gerezani kwa karibu mwaka sasa wakati hawajahukumiwa kwa lolote baya? Ni nani aliye masuul wa kadhia zinazowakuta watoto na familia za masheikh hawa katika kipindi ambacho baba, wajomba na walezi wao wanahilikika gerezani pasina kuthibitishwa kuwa wametenda kosa lolote?

Jeshi la Polisi ndilo lililoanzisha mchezo mbaya wa kuchochea wafuasi wa Uamsho kujilinda na kulinda viongozi wao. Kabla ya mchezo mbaya huo wa Polisi, Uamsho walishafanya mikutano yapata 100 kote Unguja na Pemba na Kamishna Mussa laiti kama angefuatilia yanayotokea hakuna aliyeguswa. Afghanistan, Pakistan, Yemen, Irak, Libya, Somalia na KeIlikuaje mikutano ya wakati kazi kubwa ishafanywa nya, angefikiri mara mbili kabla ya kufikiria kupanga kutoka ikumbwe na vurugu? Inasikitisha kuwa watendaji kama Kambele ya waandishi wa habari na kusema Zanzibar kuna mishna Mussa wanaona yale yaliyotokea nchini ni madogo watu wanatumiwa na makundi ya Al-Qaida na Al-Shakwa hivyo ni bora kutafuta makubwa zaidi. baab. Na iwapo Kamishna Mussa anadhani hilo ni sahihi, na alichokisimamia ni haki, basi asubiri mguso mbaya kwa Simbishii Kamishna Mussa ila nataka kumtanabahisha Zanzibar kufuatia matamshi yake ya kuwa ina watu wakuwa alichokifanya ni kitu kibaya na kitaigharimu Zanzibar, naoshirikiana na makundi maovu ya Al-Qaida na AlShanchi ambayo tayari imesingiziwa majanga mengi yakiwemo baab. yaliyosababishwa na ulegevu wake yeye kama mkuu wa

SOMA JARIDA LA ZANZIBAR DAIMA ONLINE KILA WIKI MBILI


UKURASA PAGE

36

UKURASA

37

ZANZIBAR Y O U R D A I M A H NEL IRN E O

LO G O

JAR IDA LA KILA MZAN ZIBARI


www.zanzibardaima.net Toleo 04 - 2013

MAZUNGUMZO BAADA YA HABARI

J AR I DA LA KILA MZA NZIBA RI


www.zanzibardaima.net Toleo 04 - 2013

ZANZIBAR D A I M A ONLINE

UVUMILIVU

Uhindu,Ukristo, Uislamu na dini nyenginezo zimekuwapo Zanzibar kwa miaka kadhaa na hazijawahi kukwaruzana.

Zanzibar sio limbukeni wa uvumilivu wa kidini


Na Sujae Mkiji

anzibar imekumbwa na matukio ya mfululizo ya kihalifu. Hilo halina shaka. Miongoni mwa matukio hayo yamewalenga viongozi wa kidini. Hilo ni kweli. Matukio haya hayakubaliki kufanywa wala hayavumiliki. Nalo pia ni sahihi. Matukio haya yana mkono wa kidini na au chuki dhidi ya wageni. Hilo si kweli. Kanisa la Kianglikana lililo Mkunazini lipo karibu kabisa Napinga kuhusishwa ma- na Msikiti Jibril [jina sahihi tukio haya na dini kwa saba- Msikiti Jibrin]. Adhana ikibu kadhaa. Moja ni historia adhiniwa Jibril inaingia moja na uzoefu wa nchi yetu wa kwa moja kwenye madhabakuishi karne na dahari kwa hu ya Kanisa na makengele uvumilivu mkubwa wa kidini ya Kanisa yanaingia moja na kimadhehebu, Mji Mkon- kwa moja kwenye kibla cha gwe wa Zanzibar ukiwa ni Jibril. Na hilo limekuwapo ushahidi unaotosha. kwa miaka nenda miaka rudi.

Katika mji huu uliojengwa kwenye karne ya 18 kuna misikiti 52 ya Waislamu wa madhehebu za Sunni, Ibadhi na Shia, mahekalu matatu ya Wahindu (Shree Sanatan Mandir, Hekalu la Arya Samaj na la Jain Derasa) na makanisa mawili: moja la Kianglikana na jengine la Kikatoliki.

Kanisa la Kikatoliki la Minara Miwili nalo liko karibu sana na Masjid Istiqama, ambao ni msikiti wa Ibadhi. Msikiti wa Shia Ithnaasheri wa Hamamni upo karibu kabisa na Msikiti wa Ibadhi kwa nyuma na kushoto kwake umegandana na Msikiti wa Shia Bohora wa Zenabhai. Halikadhalika mahekalu ya Wahindu yaliopo Mji Mkongwe yamezungukwa na misikiti ya Waislamu. Misikiti ya Sunni imejengwa na Shia na Ibadhi na kwenye misikiti ya Sunni wanaswali Shia na Ibadhi, huku Sunni nao wakiswali kwenye misikiti ya Shia na Ibadhi. Ardhi ya kujengea makanisa

na mahekalu ni za Waislamu na wafalme wa Zanzibar waliwapa ardhi hizo Wakristo na Wahindu wajengee nyumba zao za ibada.

chomana, kitendo ambacho ni kinyume na dini ya Kiislamu, lakini bado pande hizo mbili hushirikiana katika msiba na hufika mpaka wanapochomana Wahindu au Katika historia ya karibuni wanapozikana Waislamu. hapa Zanzibar, kuna Mkristo ambaye aliichana Quran, la- Wakristo wenye asili ya Zankini Waislamu hawakulipiza zibar huvaa mabuibui na mikisasi kwa kuchana Biblia. tandio na kanga. Na huwa Kwa hakika, kuna familia pia wanahudhuria kanisani ambazo wengine ni Waisl- wakiwa wamejitanda kanamu na wengine ni Wakristo, ga na mitandio. Ukiwaona au ambazo wengine ni Sunni masokoni, maskulini, vyuoni na wengine ni Ibadhi au Shia. na kadhalika huwezi kumjua nani Mkristo nani Mwislamu. Mkristo akifa Zanzibar, Wais- Hatutofautishwi na mavazi lamu wanahudhuria maziko- yetu. ni, na vivyo afapo Mwislamu. Wakristo wangapi Zanzibar Ramadhani ikifika tunaawamekufa mikononi mwa likana futari bila ya kujali dini Waislamu na Waislamu au madhehebu zetu. Siku za wakasimamia maziko yao Sikukuu hushirikiana pamoja kanisani mpaka wanashush- pia. Tunapelekeana vyakula wa makaburini? na Wakristo wao ikifika Pasaka na Krismasi wanatuletea Wahindu wao wakifa wana- vyakula na tunaalikana kati-

ka kumbi mbali mbali. Katika Viwanja vya kusherehekea Idd huwakuta Wahindu na Wakristo kwa pamoja wanasherehekea Idd na Waislamu. Watoto wetu wa Kiislamu tunawasomesha katika skuli za Kikristo zilizopo Zanzibar na wala Waislamu wa Zanzibar hawajawahi kusema hawawapeleki watoto wao katika skuli za Kikristo. Kwa hakika, kuna mifano pia ya watoto wa Kikristo ambao wamesoma madrassa za Quran na watoto wenzao Wakiislamu. Mitaani watoto wa dini tafauti wanacheza michezo yao pamoja bila ya kujali tafauti ya dini zao na wala watoto hawakatazwi na wazee wao wasicheze pamoja na watoto wa dini nyingine au madhehebu tafauti.
UKURASA

UKURASA PAGE

38

39

ZANZIBAR Y O U R D A I M A H NEL IRN E O

LO G O

JAR IDA LA KILA MZAN ZIBARI


www.zanzibardaima.net Toleo 04 - 2013

MAZUNGUMZO BAADA YA HABARI

J AR I DA LA KILA MZA NZIBA RI


www.zanzibardaima.net Toleo 04 - 2013

ZANZIBAR D A I M A ONLINE

Rais Mstaafu Amani Abeid Karume aliwahi kumchagua Brigadia-Jenerali Adam Mwakanyuki kuwa Waziri wa Katiba na Sheria, Wizara ambayo chini yake zipo Ofisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar na ya Kadhi Mkuu wa Zanzibar . Na Waislamu walimheshimu na hakuna Mwislamu aliyemtaka Rais amuuzulu waziri huyo katika wizara hiyo inayoratibu mambo ya Waislamu. Katika Sherehe za Kitaifa iwe za kiserikali au za kidini hualikwa Wakuu wa kidini na wa kimadhehebu kujumuika pamoja na viongozi wa kiserikali na wananchi mbali mbali. Niliwahi kupeleka wageni wangu ku-

toka Italy kutembelea sehemu za kihistoria katika Mji Mkongwe na walinambia kuwa wao wametembea nchi nyingi duniani lakini hawajawahi kuona ustahamilivu mkubwa wa kidini kama uliopo Zanzibar na wanashangaa kuona watu wanafanya ibada zao bila ya kugombana.

tumu Wakristo kuwa ndio waliofanya shambulio hilo lakini leo tunashangaa kuona ndugu zetu wa Kikristo wanawashtumu Waislamu kwa mashambulio waliofanyiwa Mapadri.

Padri kamwagiwa tindikali na kasafirishwa hapohapo, lakini Sheikh Azzan Khalid yupo hospitali mahtuti na Tunashangazwa sana kuona mafa- mpaka leo hajasafirishwa. tani wanataka kutugombanisha na ndugu zetu wa Kikristo na wa dini ny- Baadhi ya Mabalozi waliokutana engine. na Viongozi wa Uamsho wamepinga kuwa vuguvugu la Uamsho ni la Pia inawezekana matukio haya ya magaidi. watu kurushiwa tindikali ni visasi. Hatujui waliohujumiwa katika ma- Tuiache Zanzibar iendelee na safari tukio haya wamekosana nini na wen- yake na tusiyahusishe matukio haya zao. ya kihalifu na safari ya Zanzibar inapotaka kuelekea. Tusiifitinishe ZanziWaislamu wa Zanzibar alivyomwagi- bar na dunia wa tindikali Sheikh wao hawajawash-

Alama za uvumilivu wa kidini Zanzibar

BARUA ZA WASOMAJI

ZDO idumu

Assalamu alaykum Mhariri wa Zanzibar Daima Online maslahi ya biashara yao. Mara nyingi habari huwa zinaongezwa chumvi na mara nyengine zinaandikwa kwa kichukichuki hivi. Inatia moyo na kufurahisha kuona kwamba kumbe tunao waandishi wetu mahiri kwenye tasnia hii ambao wanaweza kuandika habari na makala mbali mbali zenye kuleta matumaini kwa Mzanzibari. Habari ambazo zitawasaidia Wazanzibari na hasa vijana kuweza kue-

Tafadhali naomba upoaomba nichukue fursa kee pongezi zangu kwa hii kukushukuru wewe niaba ya waandishi wako mhariri mkuu pamoja wote wanaoendelea kuna waandishi wenzako wote tuelimisha katika makala kwa kuamua kuanzisha zao mbali mbali za jarida jarida hili mliloliita Zanzihili lipatikanalo kwa kupitia bar Daima Online. Mimi ni njia ya mtandao. Tunakuwa mmoja wa miongoni mwa tunasoma habari nyingi Wazanzibari waliobahatika zinazoandikwa na magazeti kuyasoma matoleo ya maambayo mengi yanamijarida yote matatu yaliyopita likiwa na vyombo vya habari na kusema kweli nimefuvya Tanganyika. Mara nyrahishwa na makala mbali ingi wanapoandika habari mbali nilizozisoma. kuhusu Zanzibar wanaandika watakavyo wao kwa

limika kuzikimbia siasa chuki zlilizopitwa na wakati na badala yake kujielimisha kutafuta njia mbali mbali za kuweza kuleta ukombozi wa kujiletea maendeleo yao na familia zao bila kusahau maendeleo ya nchi yao. Kuna matatizo mbali mbali yanayotukabili ambayo kwa kupitia njia hii ya habari watu wetu wanaweza kujifunza njia mbali mbali za kujikwamua na matatizo haya. Ni matumaini yangu basi kuanzishwa kwa jarida hili kutakua ni njia mojawapo ya kuweza kuendelea kutuelimisha Wazanzibari popote pale tulipo. Huu ni mwanzo mzuri. Ahsanteni tena kwa jitihada zenu za kuendelea kutumia taaluma yenu kuitumikia jamii. Zanzibar Daima. Hamad London
UKURASA

UKURASA PAGE

40

41

ZANZIBAR Y O U R D A I M A H NEL IRN E O

LO G O

JAR IDA LA KILA MZAN ZIBARI


www.zanzibardaima.net Toleo 04 - 2013

TUFUNGUE KITABU

J AR I DA LA KILA MZA NZIBA RI


www.zanzibardaima.net Toleo 04 - 2013

ZANZIBAR D A I M A ONLINE

Sitiari za Mzee wa Kimbunga: Haji Gora (Sehemu ya Kwanza)


HAJI GORA HAJI
Tanbihi: Makala haya ambayo kwa mara ya mwanzo yalichapishwa kwa jina la Tungo za Bwana Kimbunga: Haji Gora Haji yameandikwa na mtaalamu wa lugha ya Kiswahili mzaliwa wa Uholanzi, PROFESA RIDDER H. SAMSOM, kuelezea kazi za kifasihi za gwiji wa sanaa ya ushairi katika zama hizi visiwani Zanzibar, Haji Gora Haji. Tunaichapisha tena hapa ikiwa imehaririwa kidogo kuakisi wakati wa sasa. Kama kokwa za fenesi, zinapochomwa jikoni Ghasiya huja upesi, na kufika mitaani Kuona hata kuhisi, ni uhuru duniyani Yavutiya vipepeo, vyenye kuruka angani Rangi nyingi zilo kwao, zinopendeza machoni Zaghilibu rangi zao, si kwa nani wala nani Ndivyo linavyositawi, asiyejuwa ni nani Lisiloweza sitawi, marejeyo sikiyeni Ni huwa au haiwi, ilivyo nitajieni Kwa hakika utungo huo aliotunga Mzee Haji katika bahari ya nyimbo unaonyesha hasa sio ubingwa wake tu, lakini pia mtindo wake na sauti yake. Nyimbo hii inatambulika kuwa imetungwa na Mzee Haji kwa sababu ya sitiari anayotumia yenye kiini cha mambo mawili kuhalifiana. Maana jiwe gani linaweza likastawi? Arudhi ya nyimbo hii, mpigo wake, mdundo wake, mizani na vituo vyake pamoja na vina - hayo yote, jinsi alivyotumia, yanaonyesha kuwa hiyo ndiyo kazi yake Mzee Haji. Sitiari nyengine anazoweka ni zile zinazotokana na mazingira yake huko Visiwani: mna mawingu na anga, mawimbi na bahmi; kuna Bwe bila wasi hufana, hufimisha tegemezi Huwanda hata kugina, ukalyona lijiezi Bwe halidumbu fana, pasipo mchinjigizi Hutaka tendelekezi, jibwe ndipo likafana Rangi zakwe za mayuwa, si haba vezo pendezi Ja mwezi unaoyawa, ukamwilika arizi Hamba macho rangi huwa, jayako weye mpezi Huburudika mtima, tondole yangu hakona Macho yano madaha, ja ya mtima simazi Huzangiwa ni furaha, hazicheleza pumuzi Ukawapo hona raha, mrembo mwenye mapozi Huburudika mtima, tondole yangu hakona Rangi nyingi za mawimbi, yazukayo kibayazi Bahari inayo dumbi, kwa kusi na kaskazi
UKURASA

vumbi na upepo, mwezi na dunia, jikoni na mitaani; kuna madakha na ghilibu; matumaini na mtihani na maisha. Haji Gora Haji ni mtu wa kisiwa cha Tumbatu, kaskazini magharibi karibu na Unguja. Tumbatu ina magofu ambayo, pamoja na Unguja Ukuu, ni ya zamani kuliko popote pengine huko Zanzibar, yaani ya karne ya tisa. Ingawa lahaja za Kitumbatu na Kimakunduchi zinahitilafiana, kuna wasomi walioziainisha pamoja katika kikundi cha lahaja za kusini. Kwa vile Mzee Haji ni Mtumbatu, anatunga kwa Kitumbatu vile vile. Kwa mfano utungo huo Jiwe Linasitawi aliutunga katika umbo la shairi kwa Kitumbatu ufuatavyo:

shairi ni mchezo. Mchezo wa maneno na hisia za watu. Katika makala haya nataka nieleze machache kuhusu tungo za Mzee Haji Gora Haji anayejulikana pia kwa jina la Mzee Kimbunga kutokana na jina la kitabu chake kilichopigwa chapa na kutolewa

1994. Nataka kutoa mifano michache ya sitiari anazozitumia, vipi zinavyohusiana na fikra kuu hiyo inayoshikiliwa na kusisitizwa na yeye mwenyewe anatambulika kama mtu gani.

Utungo ufuatao, Jiwe Linasitawi, ameutunga mnamo mwaka 1997: Na jiwe linasitawi, panapo matumaini Jiwe lisilositawi, lisiloko aridhini Ah jiwe husitawi, hilo siyo jambo geni Mauwaye yana rangi, tena nyingi naamini Ni kama mwezi sipingi, humwirika mawinguni Kama macho hizo rangi, ni yako wangu mwendani Ni macho yenye madaha, kama fikira moyoni Huingiwa na furaha, ukiwepo muhisani Ulipo huona raha, kuhisi niko peponi Rangi nyingi za mawimbi, yazukayo baharini Hwenda na kutowa vumbi, kwa upeo wa machoni Mpenzi kwako sitambi, sijiwezi taabani Ah! jamani linastawi jiwe, bali ajabu sioni Lasitawi mno jiwe, husitawishwa na nini Lisilositawi jiwe, nini wake mtihani Linanukiya upepo, unapasuwa puwani Miliyo yale ilipo, yapenya masikiyoni Maisha kimojawapo, kila siku furahani
UKURASA PAGE

42

43

ZANZIBAR Y O U R D A I M A H NEL IRN E O

LO G O

JAR IDA LA KILA MZAN ZIBARI


www.zanzibardaima.net Toleo 04 - 2013

J AR I DA LA KILA MZA NZIBA RI


www.zanzibardaima.net Toleo 04 - 2013

ZANZIBAR D A I M A ONLINE

Vikubwa vyakwe vitimbi, kingine sifananizi Kwa upeo usokoma, yanavyozuka kwayona Ahi jamani hufima, tambuyani watambuzi Hufima mno hukona, kipata naliezi Bwe velyo lisipofana, huwa lina kizuwizi Huviya penye nakama, vepo halidumbu fana Upepo linanukiya, puyani rihi ya fazi Miliyo yakwe yaliya, mashikiyo kuyahizi Maisha linaliliya, yasiwe na bumbuwazi Huviya penye nakama, vepo halidumbu fima Hamba kongwa za fenesi, zikokwa hazitikizi Hasia huja upesi, wengine kwa sana razi Kona mpaka kuhisi, uhuru wa uwamuzi Huviya penye nakama, vepo haidumbu fima Zavutiya vitunguja, virukavyo hata pazi Rangi kwao zizokuja, vezo nacho kivutizi Zahilibu kula mja, simwana wala mvyazi Hungi ni bumbuwazi, rangi hizo ukazona

LADHA YA BETI

Ningakuowa kwa Surayo


Ngekuwa mla hasara, ngeoa kwa uzurio Hawa mja wa papara, hakona hakupendao Haikosapo busara, havutiwa uzurio Leo nakiri ngeyuta, ngeoa kwa uzurio!

Moyo ulipata tabu, kuyawacha yalopendwa Hauasa sijesibu, kujidhuru sijetendwa Si bora kujisulubu, kwa mashaka yasoinda Leo unanipongeza, na raha wejionea! Hawamba wangu mtima, hawamba nisijependa Huyu kwangu sio mwema, ni bora nimwache kwenda Nipate mwenye heshima, na dini anayependa Leo najishukuria, malengo yenfikiwa! Baada kuusakama, mwisho moyo nikubali Ukinambia kwa wema, nitafute anojali Tena nioe kwa shima, nikae nae mithali Papo hajitafutia, mke nilonae sasa! Sitara niitakayo, na heshima yangu nyumba Upole wa lisaniyo, akubali ya Muumba Tabia njema utuyo, Hawaa jina loumbwa Huyu ndie mke wangu, namshukuru Muumba! Sitaki tena mwengine, wa mtima kutibua Sitaki shoti niseme, niwambie wasojua Sitaki msijipime, kwangu taka jirejea Nimesharidhika kwake, kwamwe mwengine simwebu!

Nekumbuka lipokona, mato yalipoangaza Malaika nekuona, wameta wanchichiza Hafikiri setaona, alokuzidi aziza Ningekiona cha moto, ngekuoa kwa uzurio! Akili libadilika, na moyo ukafatiza Matozi yebubujika, mtima wauumiza Henenda hajiapiza, takuoa nikifanza Ela leo nakubali, ngekuwa mla hasara! Usia ulotolewa, wazazi walonifunza Mwanamke kuolewa, kwa tabia ni aziza Si sura wala si quwa, si ukoo unojuza Ngewakana ningeyuta, mayuto ya milenia! Basi lipokumbukia, wasia niloagizwa Nekaanza kukwambia, nawe kiona wavizwa Hasira ukatukua, na maneno yasofunzwa Ela ningelazimisha, leo ngekuwa tabuni! Dini mafunzo hubiri, kwa mchumba kumwegeza Mwili wake usitiri, na ngoma asijecheza Papo ugomvi shamiri, na matusi kichombezwa Wazazi walinipenda, tawashukuru daima

Haji Gora Haji amezaliwa mwaka 1933 kijiji cha Kokoni huko Tumbatu. Alipokuwa na umri wa miaka mitano tu alichukuliwa na akakulia huko Mkunazini, mtaa wa katikati ya Zanzibar Mjini.

wa majahazi yaliyopitia mwambao wote wa Afrika ya Mashariki. Naye Haji Gora mwenyewe tangu alipoanza kuvua, maisha yake yote hadi sasa yamehusiana na bahari akiwa mvuvi, baharia, mpagazi na mchukuzi bandarini, msafirishaji wa karafuu na mwajiriwa wa Hapo mjini alikuwa akisoma dini chuoni, lakini kampuni ya Kichina huko Tanga aliyoitafutia hakupata fursa ya kwenda skuli ya serikali majongoo ya ufukweni. maana ilimbidi aanze kufanya kazi akiwa bado mdogo. Akafundishwa na mjomba Alipokuwa na miaka 16 alijiunga na kikundi wake, Haji Mjumbe, uvuvi wa nyavu na baacha vijana kilichojiita Ujinga Mwingi huko daye baba yake mdogo, Pandu Haji, alimpa Tumbatu na kuanza kujihusisha na ngoma. ujuzi wa uvuvi wa madema. Kama desturi ngoma za aina hii, hushindana kwa kutungiana mashairi na kuyaimba hadBaba yake alikuwa baharia hodari na nahodha harani, kulumbana na kujibizana.
UKURASA PAGE

Othman Ali Haji Zanzibar

44

UKURASA

45

ZANZIBAR Y O U R D A I M A H NEL IRN E O

LO G O

JAR IDA LA KILA MZAN ZIBARI


www.zanzibardaima.net Toleo 04 - 2013

Lazima tujiangalie wenyewe


Muungano na Mzee Joseph Butiku, aliyekuwa karibu sana na Mwalimu Julius Nyerere alipokuwa Katibu Mkuu Ikulu, ilikuwa sawa na mdogo kulalamika kwa mkubwa. Lakini huo ni upande mmoja wa kadhia yenyewe upande wa namna Zanzibar inavyoonewa na mshirika mwenzake wa Muungano, Tanzania Bara. Kuna upande mwengine wa suala hili nao ni wetu wenyewe kama Wazanzibari na hasa zaidi viongozi wetu tuliowapa dhamana ya kutusimamia na kutuongoza. Je, baada ya kadhia zote mbili viongozi hao wahusika walifanya nini? Na laiti hakungekuweko na warsha na majukwaa ya kuweza kujieleza, wangekuwa na ubavu wa kuyazungumza hadharani?

NIONAVYO

Mwanasiasa mwadilifu ni yule mwenye ujasiri wa kusema kitu kisichowapendeza wengine, ilimradi awe mkweli. Akikosoa awe anakosoa kwa kujenga na sio kubomoa na awe na moyo wa kueleza na kufichua hadharani tatizo linaloihusu jamii na kuipa jamii nafasi ya kuchangia katika kutafuta suluhisho. Kwa bahati mbaya miongoni mwa wanasiasa tulionao katika Chama cha Mapinduzi (CCM), chama chenye kutawala, kuna wasio na ujasiri huo. Huenda hawa wakawa ndio wengi na wanapojitokeza baadhi ya wakati hadharani huwa zaidi ni kujitoa kimasomaso tu. Sababu kubwa labda inayowafanya wawe hivyo ni haja ya kuyalinda masilahi yao binafsi. Nimekuwa nikipitiapitia vidio za matukio ya kisiasa ya Zanzibar katika mtandao wa
UKURASA PAGE

Na Mohamed Abdul-Rahman

YouTube na nikazikuta za mawaziri wawili wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) wakiuzungumza Muungano. Mawaziri hao waliokuwa wakizungumza katika nyakati mbali mbali kuhusu kero za Muungano na jinsi Zanzibar inavyokandamizwa ni Waziri wa Fedha, Omar Yusuf Mzee, aliyekuwa akizungumza katika semina ya Baraza la Wawakilishi. Mwengine ni Mwinyihaji Makame aliyekuwa akitoa maoni katika Tume ya Katiba ya Jaji Joseph Warioba. Walioyaeleza yanatia unyonge, yanakereketa na yanasikitisha. Yusuf Mzee alitaja kisa kilichotokea wakati wa mkutano wa Utalii Katika Nchi za Visiwa uliofanywa Mauritius. Ujumbe uliokwenda huko uliongozwa na Waziri

Waziri wa Nchi Afisi ya Rais, Mwinyihaji Makame.


Ali Juma Shamhuna ambaye alilakiwa kama viongozi wa jumbe zote nyingine na alipewa heshima alizostahiki. Hata hivyo, kwa mujibu wa Yusuf Mzee, siku ya pili uliwasili ujumbe wa Tanzania Bara na kuanzia wakati huo Mheshimiwa Shamhuna alinyanganywa gari na gari hilo akapewa Waziri wa Serikali ya Muungano na yeye Shamhuna akajiunga na wengine akiwa sehemu tu ya ujumbe. Swali alilouliza Mzee lilikuwa Tangu lini Bara ikawa nayo ni kisiwa? Sijui kama Waziri Shamhuna alimuuliza mwenzakewa Bara swali hilo baada ya hayo kutokea. Manunguniko ya Waziri Makame nayo yalihusiana na utiaji saini nyaraka mbili tafauti, waraka mmoja wa Muungano na mwingine wa Zanzibar wakati wa ziara moja ya nchi za nje wakiwa katika ujumbe wa Rais wa Jamhuri ya Muungano, Jakaya Kikwete. Kwa mujibu wa itifaki ilikuwa aanze Waziri wa Mambo ya Nje, Benard Membe, na baadaye yeye Makame kwa niaba ya Zanzibar. Kiroja cha mambo ni kwamba Membe alizitia saini nyaraka

zote mbili. Kwa masikitiko Makame alisema alimuuliza Membe na akajibiwa You have no instruments ikiwa na maana Makame hakuwa na mamlaka (madaraka) ya Bila shaka waliyadhukuru kwa kutia saini nyaraka iliyohusu sababu palitolewa rukhsa na Zanzibar. wakawa na fursa ya kutoadukuduku lao kadamnasi. Kwa Yeyote aliyeiona kanda hiyo kufanya hivyo, umma wa Wana kuyasikia yaliyosemwa zanzibari umewaona walivyo atakubaliana nami kuwa ya- washupavu kwa ajili ya nchi likuwa mambo mazito na ye- yao. Lakini je, ni kweli kwamnye kuhuzunisha. ba uthubutu huo wanao kwenye vikao vyao vya ndani, pale Yaliyomkuta Makame ndiyo viongozi wa Bara kwa jina la yaliyonisikitisha zaidi kwani Muungano wanapowakabili? alipokuwa akielezea yaliomsi- Kama wanao, mbona hatuoni bu mbele ya Warioba aliyewa- kinachobadilika? hi kuwa Mwanasheria Mkuu na Waziri Mkuu wa Serikali ya Nionavyo, majibu ya maswali haya

46

UKURASA

47

ZANZIBAR Y O U R D A I M A H NEL IRN E O

LO G O

JAR IDA LA KILA MZAN ZIBARI


www.zanzibardaima.net Toleo 04 - 2013

NIONAVYO
Waliojitokeza kuitetea Zanzibar kwa kutoshirikishwa ni vyama vya upinzani CHADEMA, CUF na NCCR-Mageuzi. Wabunge wa CCM Zanzibar akiwemo Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Iddi, walilipa mgongo suala hilo na walikibariki kile kinacholalamikiwa na taasisi kadhaa huru nchini Tanzania kwamba ni upotoshaji. Mansoor amewapa somo na mwangaza wenzake alokuwa nao katika CCM kwa kuwakumbusha yafuatayo:

yanahitajika sana ili wananchi wasiendelee kufanywa waamini kwamba uongozi wetu wa Zanzibar ni kielelezo cha udhaifu na unyonge mbele ya Bara. Uongozi unaotishiwa kwa chui wa karatasi, ukaufyata mkia katikati ya mapaja. Hofu iliyopo ni kwamba uongozi wa Zanzibar umekosa nia ya kweli na ujasiri wa kuitetea Zanzibar kwa uwazi bila ya woga au kificho. Huenda baadhi wakawa na maoni tafauti kwamba kuna mawaziri na wajumbe wa Baraza wasio katika kundi hilo, lakini ushahidi wa wazi ni kuwa ni wachache wenye ujasiri wa kina Mansoor Yusuf Himidi, Mwanasheria Mkuu Othman Masoud, Mkurugenzi wa Mashtaka Ibrahim Mzee au Mwakilishi Mohamed Raza.

1. Mwanasiasa mwadilifu ni yule anayesimamia haki na ukweli daima. Hili limesisitizwa na mwongozo wa CCM yenyewe kwa maneno haya: Nitasema kweli daima fitina kwangu mwiko. Lau tungekuwa na hawa 10 kwenye safu ya juu ya uon- 2. Jukumu la mwanasiasa ni kuwaongoza waliomchagua gozi, basi hadithi yetu ingelikuwa tafauti hivi leo. kwa kutetea matakwa yao. Badala yake kinachoshuhudiwa huko juu ni woga, hofu 3. Vyama huja na kuondoka lakini taifa linabakia. na kutoana vikoa kwa pupa ya kunusuru masilahi binafsi, kwa jina la kulinda sera za chama. Kwa mfano tukichuku- Wanalopaswa viongozi wa Zanzibar kulizingatia ni lia kisa cha Mansoor kufukuzwa CCM, karibu nusu ya wa- kwamba macho ya waliowachagua yanawamurika na ni jumbe wa Baraza la Mapinduzi kutoka CCM ni wajumbe misimamo yao ndiyo itakayowaweka wanapostahili kuwa Kamati Maalum ya chama hicho upande wa Zanzibar. wekwa katika historia ya visiwa hivi. Lakini ni wachache mno waliojitokeza kumtetea Mansoor. Hapa siwazungumzi wanasiasa wa CCM pekee bali hata Kadhia nyengine ni mvutano uliozuka karibuni katika wale wa chama cha CUF wenye kufikiria matumbo yao tu. bunge la Muungano Dodoma kuhusu Rasimu ya Katiba na mizengwe iliyofanywa na chama kinachotawala kub- Namkumbuka mzee wangu mmoja aliyeniambia kuwa adilisha sehemu ya yaliomo ndani ya Rasimu hiyo. siasa ya mwongo ni uwongo, ya fatani ni fitna na ya mkweli ni ukweli, lakini huu ukweli unahitaji ujasiri.

Waziri wa Fedha Zanzibar, Omar Yussuf Mzee.

UNAWEZA PIA KULISOMA ZANZIBAR DAIMA ONLINE KUPITIA MITANDAO YETU YA KIJAMII FACEBOOK/ZANZIBARDAIMALTD

UKURASA PAGE

48

UKURASA

49

ZANZIBAR Y O U R D A I M A H NEL IRN E O

LO G O

JAR IDA LA KILA MZAN ZIBARI


www.zanzibardaima.net Toleo 04 - 2013

MICHEZO

J AR I DA LA KILA MZA NZIBA RI


www.zanzibardaima.net Toleo 04 - 2013

ZANZIBAR D A I M A ONLINE

Zanzibar ina uwezo wa kusonga mbele kwenye soka

Na David Kambona

uendeshaji soka ya vyama vingine duniani hasa katika ambo moja nataka suala la kikatiba. Hiyo ni niliseme wazi kabla ya sehemu iliyo muhimu katika kuendelea na makala sheria ya chama chochote haya. Mimi si Mzanzibari, kile cha soka duniani. Hili ni ni Mtanzania kutoka Bara jambo linaloweza kufanywa lakini linapokuja suala la hata katika muda wa miaka kimaendeleo huwa siangilii mitatu au mitano. nina asili ya wapi, bali huwa Jambo la pili baada ya suala ninaangalia bara ninalotoka. la kikatiba, ZFA itatakiwa Zanzibar inaweza kuviondo- kukaa na vilabu vyote vinaNchi yoyote ile kutoka Afsha vizingiti hivyo kiurahisi vyoshiriki ligi ya Zanzibar rika nitaiunga mkono. Huwa tena bila ta kutumia nguvu. bila kujali daraja, ili vijadilnaamini mimi ni Mwafrika Katika uongozi wa ZFA yapo iane aina ya mfumo wa ligi na ninawajibika kuwasaidia mengi sana ya kimsingi na aina ya uendeshwaji ligi Waafrika wenzangu. Huo yanayotakiwa kwanza ya Zanzibar. ndio msingi wa kuandika yafanywe kabla ya kwenda kwangu. kujiunga na FIFA. Wakati huo huo, vilabu kwa kushiriakina na wadau wa Tena mimi huwa nasikia Kwanza ni kuondoa misoka wa Zanzibar wataraha nikiwa Zanzibar hasa vutano isiyokuwa na tija tikiwa kutazama ni jinsi gani Bwawani au Forodhani yoyote kwa viongozi wa wanaweza kutengeneza kwa sababu katika sehZFA toka Unguja na Pemba miundombinu ya soka ya emu hizi ukipita huwezi kukaa pamoja na kugawana Zanzibar ili iweze kutoa kusikia mindundo ya muziki mambo ya kitaasisi nusu wachezaji wenye uwezo na kutoka nje ya Zanzibar au kwa nusu bila kujali ukubwa vipaji vikubwa. muziki wa Kimagharibi hasa wa kisiwa kimoja au kingine. nyakati za usiku. Lazima Ikiwa sasa ambapo Zanziutasikia muziki maridhawa Soka ni mchezo unaobar haina hata academy wa Taarab. pendwa zaidi Zanzibar na na wachezaji wake wana ulimwengu kwa ujumla kwa uwezo wa kucheza kwenye Kwa kweli ipo haja ya kuan- sasa visiwa vya Unguja na vikosi vya timu za Bara, je za kuthamini vya kwetu Pemba Vinatakiwa kuijenga kukiwa na shule za soka haya mimi natoka Bara ZFA kuwa taasisi inayotitakuaje? tena Mnyasa wa Mbabay ambulika ndani ya Zanzibar Kwambe kijiji alichozaliwa bila kujali uwepo wa TFF Ukiwa na shule nne - mbili mmoja kati ya viongozi wa kwa Tanzania ambayo ndiyo Unguja na mbili Pemba na Tanzania Oscar Kambona taasisi inayotambuliwa na zikawa na usimamizi mzuri, lakini ninaweza kuyaona FIFA, CAF. katika muda wa miaka 10 haya Zanzibar. ijayo lazima tutaona moja Kwa kuijenga ZFA itatakiwa katika ya vilabu vya ZanWazanzibari wengi wamekutazama mifumo mipya ya zibar vinashiriki katika ligi

kuwa wapweke sana kwa kunyimwa haki yao ya kimsingi ya kutaka kutambuliwa na Shirikisho la kimataifa la Soka Duniani (Fifa) huku wakipata nafasi ya uangalizi kwa kutambuliwa na shirikisho la soka Afrika, CAF, kupitia chama cha soka cha nchi hiyo, ZFA.

Kikosi cha timu ya Taifa ya Zanzibar ya Mabingwa wa Afrika kwa hatua ya robo fainali. Tunaweza sema kuwa soka ya Zanzibar inahitaji mageuzi ya kimsingi kwa kuitazama tena upya soka. Ninaamini inawezekana. Hata kama watu wanasema Zanzibar haitambuliki, ipo siku wataitambua kwa kufungwa na Zanzibar, kwani hata siku Zanzibar ilipotwaa kombe la Challenge ninaamini ya kuwa Afrika ya Mashariki ilitambulika. Haiwezekani nchi kama Cape Verde na nyengine ndogo za visiwa zishiriki mashindano ya mataifa ya Afrika, lakini Zanzibar ishindwe. Kwa hiyo natoa rai yangu kuwa tuanze sasa kuutazama mfumo wetu na tuurekebishe. Tujiulize, je unaendana na FiFA, CAF, CECAFA? Kinachotakiwa kwa Zanzibar ni kusimamisha mchezo mmoja kwanza kama zilivyo kwa nchi nyingine ambazo zimediriki kusimamisha mchezo mmoja. Mfano ni riadha kwa Kenya na Ethiopia. Kwa maana hii lazima tufe kwanza ili tufanikiwe sehemu tunayotaka kwenda. Haitakuwa jambo rahisi kutaka kutambulika Fifa kama mambo ya msingi katika michezo hatutayawekea misingi imara. Kwa Zanzibar ambayo imepata kutambulika japo sio rasmi katika CAF ukifanya majumuisho unaweza kuona kabisa ya kuwa bado hatujafika katika kiwango hata cha kufuzu duru ya pili ya mashindano ya kimataifa . Endapo tutatengeneza misingi katika taasisi kubwa ya kimichezo kama ZFA na pindi itakaposimama yenyewe ndipo vyama vingine vinaweza kusimama kwa kufuata usimamizi wa ZAF. Mfano kwa sasa ukitazama kimiundo mbinu ya michezo hata uwanja wa Mao Tse Tung hauridhishi katika viwango stahiki vya kimataifa. Je, utaitaka vipi Zanzibar itambuliwe na Fifa wakati mambo yetu hayajakaa sawa?

UKURASA PAGE

50

UKURASA

51

Das könnte Ihnen auch gefallen