Sie sind auf Seite 1von 1

Rai /Alhamisi Oktoba 2-8, 2014

2
HABARI
NA MWANDISHI WETU
M
OJA ya kashfa inayotajwa
kulitesa Taifa kwa sasa na huenda
ikaitingisha kwa kiasi kikubwa
Serikali, ni ile ya ukwapuaji wa kiasi cha
Sh. bilioni 200 kutoka kwenye akaunti ya
Escrow iliyoihusisha kampuni ya kufua
umeme ya Independent Power Tanzania Ltd
(IPTL) na Shirika la Ugavi wa Umeme nchini
(Tanesco).
Kashfa hiyo ambayo ilijadiliwa kwa kiasi
kikubwa kwenye Bunge la Bajeti la mwaka
huu, iliibua mjadala mzito uliosababisha
pande zinazosigana kufikishana mahakani,
huku Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali
(CAG) akipewa jukumu la kuchunguza saka-
ta hilo.
Madai ya ukwapuaji wa fedha hizo ya-
naelekezwa moja kwa moja kwa baadhi ya
watendaji wa juu serikalini ambao wanata-
jwa kushirikiana na mwekezaji ambaye ina-
daiwa umiliki wake wa IPTL umejaa utata.
Utetezi na vitisho vilivyokuwa vikitolewa
na baadhi ya watendaji wa Serikali juu ya
wabunge waliokuwa wakilipigia kelele su-
ala hilo unatajwa kuuaminisha umma kuwa
wakubwa hao wamehusika na kwamba wana-
fanya jitihada za kuuficha ukweli wa jambo
hilo ambalo hivi karibuni liliingia kwenye
vichwa vya habari vya gazeti la African Confi-
dential la Uingereza.
Pamoja na jitihada hizo za kutaka ukweli
kufichwa, mambo yanaonekana kwenda
kombo kwani hivi karibuni ukweli utabaini-
ka.
Ukweli huo utabainika kutokana na ri-
poti uchunguzi ya CAG kukamilika, ambapo
inatajwa kubaini madudu ya hatari ambayo
yanatishia uimara wa Serikali ya awamu ya
nne.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesa-
bu za Serikali (PAC), Zitto Kabwe, ameliam-
bia RAI kuwa ripoti hiyo itaingia mikononi
mwake wiki hii.
Hatua ya Zitto kukabidhiwa ripoti hiyo
inakuja kufuatia agizo la Kamati yake Machi
20, mwaka huu kumtaka CAG kufanya
uchunguzi wa kina wa sakata hilo.
PAC ilimtaka CAG kuchunguza kama
akaunti hiyo iliihusisha Kampuni ya Mech-
mar iliyokuwa na hisa za umiliki katika Kam-
puni ya IPTL.
Aidha alitakiwa kuthibitisha kama Mech-
mar ilikuwa imehamisha umiliki wake kwen-
da kampuni ya Pan African Power Solution
(PAP) kabla ya kufilisiwa.
Pia CAG alitakiwa kuchunguza kiwango
cha fedha kilichopaswa kuwapo kwenye
akaunti ya Escrow wakati Benki Kuu ina-
hamisha fedha hizo kwenda IPTL.
Pamoja na mambo mengine lakini pia,
CAG alipewa jukumu la kuchunguza na kutoa
taarifa kuhusu kiasi cha fedha kilichowekwa
na kila mhusika hadi siku uamuzi wa Ma-
hakama Kuu kuhusu kesi hiyo ulipotolewa.
Jukumu jingine lilikuwa ni kuchunguza
madai ya Benki ya Standard Chartered (Hong
kong) kwa IPTL na madai mengine ya kuzali-
sha umeme wa IPTL na kama Serikali iliji-
hadhari na uwezekano wa madai yanayoweza
kufunguliwa dhidi yake na wadai mbalimbali.
Pia CAG alitakiwa kuchunguza uadilifu wa
Wizara ya Nishati na Madini ambayo iliingia
mkataba na IPTL kufungua akaunti hiyo na
kuweka uangalizi kabla ya kutoa fedha zi-
lizokuwapo kwenye akaunti hiyo.
Katika kuusaka ukweli wa jambo hilo CAG
alitakiwa kufanya uchunguzi kuhusu hisa za
Mechmar iliyotajwa kufilisika huku ikidaiwa
kuwa na hisa nyingi za IPTL.
Aidha alitakiwa kuangalia kama hisa hizo
sasa zinamilikiwa na PAP, ambapo alipewa
jukumu la kutoa mapendekezo ya njia sa-
hihi za kisheria zinazoweza kutumika kwa
ajili ya kulinda Serikali isipate hasara katika
utekelezaji mkataba wa IPTL.
PAC ilimtaka CAG kufanya ukaguzi kwe-
nye shughuli zote za uhamishaji fedha zi-
lizofanyika Julai Mosi, 2006 hadi Machi 31,
mwaka huu.
Akizungumzia majukumu hayo aliyopewa
CAG, Zitto alisema yametekelezwa kwa ufani-
si mkubwa na kwamba ripoti hiyo ikiwekwa
hadharani haitaiacha salama Serikali.
Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma
Kaskazini (Chadema), alisema kutokana na
unyeti wa sakata lenyewe na ripoti ya CAG,
hali inaonesha kuwa mbaya kwa serikali ku-
tokana na vielelezo vilivyokusanywa na CAG.
Kazi hii tayari CAG ameifanya na atani-
kabidhi ripoti hiyo wiki ijayo (wiki hii), sisi
tutaishughulikia kwenye Kamati na kuiwasil-
isha kwenye vikao vya Bunge la mwezi No-
vemba mwaka huu.
Tayari nimeshapokea ripoti maalum ya
jengo la wageni maarufu kwenye uwanja wa
ndege Kimataifa wa Dar es Salaam. Ujenzi
wake umegharimu Sh. bilioni 12, ambazo ni
sawa dola za Marekani milioni nane, kati ya
hizo dola milioni tano ni msaada kutoka kwe-
nye shirika moja la China na dola milioni tatu
zilitoka Serikalini.
Tunapokea ripoti nyingi, lakini hii ya
IPTL ni nzito zaidi. Oktoba 20, mwaka huu
tumemuita Gavana wa Benki Kuu kwenye
Kamati, naamini hii ripoti itawashangaza
wengi, niliagiza ukaguzi wa vyama vya siasa
kwenye upande wa ruzuku, tunatarajia pia
kupokea taarifa hiyo na tutamwita msajili wa
vyama vya siasa.
Pia kuna tatizo la mifuko ya hifadhi ya
jamii, tumemwita mjumbe wa SSRA wote
watakuja, nawahakikishia Watanzania ripoti
hii ya IPTL inaweza kuiangusha serikali,
alisema.
Tayari sakata hilo limemuibua Waziri wa
Ardhi, Nyumba na Makazi, Profesa Anna
Tibaijuka ambaye amekiri kupokea kiasi cha
Sh. bilioni moja ambazo amedai kuwa alipe-
wa kama mchango kwa ajili ya shule ya se-
kondari Babro.
Wadadisi wa mambo wanaamini kuwa
ripoti ya CAG ambayo inamfanano mkubwa
na ile ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana
na Rushwa nchini (Takukuru) hazitawaacha
salama baadhi ya vigogo serikalini na kwenye
taasisi kubwa za fedha nchini kutokana na
kuguswa kwao moja kwa moja.
Spika wa Bunge Anne Makinda ni mmoja
wa wanasiasa wanaoamini kuwa ripoti ya
CAG, Ludovick Utouh ambaye ametajwa
kustaafu hivi karibuni haiwezi kuwaacha
salama baadhi ya mawaziri.
Makinda aliweka wazi kuwa ripoti za Ut-
ouh zimekuwa zikiandikwa kwa umakini
mkubwa na kwamba kilichowaokoa mawaziri
walioguswa na ripoti hiyo kwa sasa ni Bunge
Maalum la Katiba.
Ripoti nyingi za Utouh zimekuwa
zikiwangoa mawaziri, naamini hata hii ya
IPTL itaondoka na watu, kwa sasa baadhi ya
mawaziri wameokolewa na Bunge Maalum
la Katiba,alinukuliwa Makinda wakati wa
hafla ya kumuaga Utouh.
Zitto: Ripoti ya IPTL kuiangusha Serikali
Jukumu jingine
lilikuwa ni
kuchunguza
madai ya Benki
ya Standard
Chartered
(Hong kong)
kwa IPTL na
madai mengine
ya kuzalisha
umeme wa
IPTL na
kama Serikali
ilijihadhari na
uwezekano
wa madai
yanayoweza
kufunguliwa
dhidi yake
na wadai
mbalimbali.
Pia CAG alitakiwa kuchunguza
kiwango cha fedha kilichopaswa
kuwapo kwenye akaunti ya
Escrow wakati Benki Kuu
inahamisha fedha hizo kwenda
IPTL.

Das könnte Ihnen auch gefallen