MWALIKO KWA WENYE NIA YA KUNUNUA HISA NA KUWEKEZA MTAJI

KWENYE BENKI YA TWIGA
Kwa mamlaka iliyopewa kisheria kupitia kifungu namba 56(1) (g) (i) cha Sheria ya
Mabenki na Taasisi za Fedha ya mwaka 2006, Benki Kuu ya Tanzania ilichukua usimamizi
wa benki ya Twiga Bancorp Ltd (Twiga) kuanzia tarehe 28 Oktoba, 2016.
Hatua hii ilichukuliwa baada ya kubainika kuwa benki ya Twiga ilikuwa na upungufu
mkubwa wa mtaji kinyume na vigezo vilivyoainishwa kwenye Sheria ya Mabenki na
Taasisi za Fedha ya 2006 na kanuni zake. Aidha, kuendelea kufanya biashara katika hali hii
kungehatarisha uthabiti wa sekta ya fedha, maslahi ya wenye amana na wadai wengine.
Kwa mamlaka iliyopewa chini ya kifungu cha 58(2)(i) cha Sheria ya Mabenki na Taasisi za
Fedha ya 2006, Benki Kuu ya Tanzania imeamua kutatua tatizo la upungufu wa mtaji kwa
kuwakaribisha wenye nia ya kununua hisa na kuleta mtaji kwenye benki hii. Kwa
kuzingatia kifungu cha 59(6) cha Sheria ya Mabenki na Taasisi za Fedha ya 2006, Benki
Kuu ya Tanzania inawaalika watu binafsi na makampuni ya ndani na nje ya nchi wenye nia
ya kununua hisa na kuleta mtaji mpya kwenye benki ya Twiga, kuwasilisha maombi yao
Benki Kuu ya Tanzania.
Maombi hayo yawasilishwe kwa Gavana, Benki Kuu ya Tanzania, 2 Mtaa wa Mirambo,
11884 Dar es Salaam. Maombi yawasilishwe kwa maandishi yakiwa yameandikwa
“Mwaliko kwa Wenye Nia ya Kununua Hisa na Kuwekeza Mtaji Kwenye Benki ya
Twiga”. Mwisho wa kupokea maombi ni siku ya Ijumaa, tarehe 11 Novemba 2016 kabla ya
saa 10.30 jioni. Watakaotimiza vigezo wataalikwa kufanya upembuzi wa hali ya kifedha ya
benki ya Twiga hadi kufikia Ijumaa tarehe 18 Novemba 2016 ili kutoa nafasi kwa hatua
zingine kuendelea. Utoaji wa taarifa za mahesabu kwa ajili ya kufanya upembuzi yakinifu
wa hali ya fedha ya Twiga utafanyika baada ya kusaini Makubaliano ya Kuhifadhi Siri
(Confidentiality Agreement).
Kwa maelezo zaidi wasiliana na Mkurugenzi wa Usimamizi wa Mabenki kwa simu namba
+255 22 2235483, nukushi +255 22 2234189 au barua pepe kanyoni@bot.go.tz.
BENKI KUU YA TANZANIA
8 NOVEMBA 2016

NOTICE TO THE PUBLIC
INVITATION TO EXPRESS INTEREST TO ACQUIRE SHARES AND PUT IN
NEW CAPITAL INTO TWIGA BANCORP LIMITED
In exercising its powers under sections 56(1)(g)(i) and 56(2) (a)-(d) of the Banking and
Financial Institutions Act, 2006, Bank of Tanzania effective 28 th October, 2016 took
over the administration of Twiga Bancorp Limited (Twiga).
This measure was taken upon determination by Bank of Tanzania that Twiga is a
significantly undercapitalised institution as provided under the Banking and Financial
Institutions Act, 2006 and its regulations. This poses a systemic risk to the stability of
the financial system and that the continuation of Twiga operations in its current capital
position is detrimental to the interest of its depositors and other creditors.
As authorized under section 58(2)(i) of the Banking and Financial Institutions Act,
2006, Bank of Tanzania has resolved to reorganize ownership of Twiga to address the
problem of undercapitalization by inviting interested entities and individuals to acquire
shares and inject capital in Twiga. Accordingly, as required under section 59(6) of the
Banking and Financial Institutions Act, 2006, Bank of Tanzania hereby invites
interested entities and individuals, either local or foreign, to express interest to acquire
shares and put in new capital into Twiga.
Interested parties should submit to the Governor, Bank of Tanzania, 2 Mirambo Street,
11884 Dar es Salaam, Tanzania, their written expression of interest in English to be
titled “Expression of Interest to Acquire Shares and Put in New Capital into Twiga”
not later than Friday 11th November 2016 before 1630 hours East African time. After
receipt and evaluation of the Expressions of Interest, pre-selected entities and/or
individuals re-selected entities and individuals will be required to conclude due
diligence of financial position of Twiga by Friday 18th November 2016. Disclosure of
financial position of Twiga to pre-selected parties shall be subject to signing of
Confidentiality Agreement.
For further clarification, interested parties may contact Director Banking Supervision,
Bank of Tanzania, telephone number +255 22 2235483, fax number +255 22 2234189
or through email - kanyoni@bot.go.tz.
BANK OF TANZANIA
8th November 2016