Sie sind auf Seite 1von 4

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI


JESHI LA POLISI TANZANIA

TELEGRAMS: POLISI,
TELEPHONE: 2500712
Fax: 2502310
E-mail: mwapol@yahoo.com
rpc.mwanza@tpf.go.tz

OFISI YA
KAMANDA WA POLISI,
MKOA WA MWANZA,
S.L.P. 120,
MWANZA.

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA KWA


VYOMBO
VYA HABARI LEO TAREHE 9.01.2016

WATU WAWILI WAMEFARIKI DUNIA NA WENGINE WATATU KUJERUHIWA


KATIKA AJALI YA GARI ILIYOHUSISHA ROLI LA MIZIGO NA GARI DOGO
AINA YA SUBARU FORESTER SALOON WILAYANI MAGU.

MTU MMOJA AMEFARIKI DUNIA BAADA YA KUGONGWA NA GARI


WILAYANI MISUNGWI.

KWAMBA MNAMO TAREHE 8.01.2017 MAJIRA YA SAA 06:10HRS ASUBUHI KATIKA


KIJIJI CHA KISESA ENEO LA KONA YA KAYEZE BARABARA YA MWANZA
MUSOMA WILAYANI MAGU MKOA WA MWANZA, WATU WAWILI WALIOJULIKANA
KWA MAJINA YA 1. DANIEL JOACKIM @ NYAMBO MIAKA 33, MFIPA NA 2. JANET
ADEN @ KAGOSA MIAKA 22, MJALUO, WAMEFARIKI DUNIA PAPO HAPO NA
WENGINE WATATU KUJERUHIWA KATIKA AJALI YA GARI ILIYOHUSIAHA LORI LA
MIZIGO LENYE NAMBA T.575 BAT AINA YA SCANIA TRUCK LENYE TELA LENYE
NAMBA 270 AKK LILILOGONGANA NA GARI DOGO LENYE NAMBA T. 480 CAS AINA
YA SUBARU FORESTA SALOON LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA AITWAYE
DANIEL JOACKIM AMBAYE ALIFARIKI DUNIA KATIKA AJALI HIYO.
MAJERUHI WA AJALI HIYO NI 1. ADEN KAGORA MIAKA 55, MJALUO, 2. MICHAEL
JOSEPHAT KAGOSA MIAKA 15 NA 3. VICTORIA KAGOSA MJALUO MIAKA 13, WOTE
NI ABAIRI WA GARI NDOGO LENYE NAMABA T. 480 AINA YA SUBARU FORESTA
SALOON, AIDHA HAKUNA DEREVA AU ABIRIA WA LORI ALIYE JERURIHIWA AU
KUPOTEZA MAISHA KATIKA AJALI HIYO.
CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI WA DEREVA WA GARI DOGO AMBAYE
ALISHINDWA KULIMUDU GARI ALIPOKUWA KWENYE KONA YA ENEO LA KAYEZE
NA KUSABABISHA AJALI, MAJEERUHI WAMELAZWA HOSPITALI YA RUFAA YA
BUGANDO NA HALI ZAO ZINAENDELEA VIZURI, MIILI YA MAREHEMU PIA
IMEHIFADHIWA HOSPITALINI HAPO PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA
ITAKABIDHIWA KWA NDUGU WA MAREHEMU KWA AJILI YA MAZISHI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED
MSANGI ANATOA RAI KWA WAENDESHAJI WA VYOMBO VYA MOTO AKIWATAKA
KUWA MAKINI WAKIZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI
PINDI WANAPOKUWA BARABARANI ILI KUEPUKA VIFO NA AJALI ZINAZOWEZA
KUEPUKIKA. AIDHA ALIWATAKA ABIRI KUTOA TAARIFA MAPEMA POLISI PINDI
WANAPOONA VIASHIRIA VYA MWENDO KASI ILI HATUA ZICHUKULIWE HARAKA
KABLA MADHARA HAYAJATOKEA.

KATIKA TUKIO LA PILI

KWAMBA TAREHE 08.01.2017 MAJIRA YA 22.30HRS USIKU KATIKA BARABARA YA


MWANZA SHINYANGA ENEO LA KIKIJI CHA USAGARA KATA NA TARAFA YA
USAGARA WILAYA YA MISUNGWI MKOA WA MWANZA, GARI NAMBA SU 40653
AINA YA TOYOTA HILUX MALI YA SHIRIKA LA TENESCO MKOA WA MWANZA
LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA AITWAYE WEREMA IKWEBE MIAKA 35
MKAZI WA IGOGO TANESCO LIKITOKEA MWANZA KWENDA
SHINYANGA
LILIMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU AMBAYE HAJAFAHAMIKA JINA WALA
MAKAZI ANAYEKADIRIWA KUWA NA UMRI KATI YA MIAKA 50 HADI 55, WAKATI
AKIVUKA BARABARA NA KUFARIKI DUNIA PAPO HAPO.
CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI WA DEREVA GARI ALIYESHINDWA
KULIMUDU GARI NA KUSABABISHA AJALI HADI KIFO, DEREVA WA GARI HILO
AMEKAMATWA PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA ATAFIKISHWA MAHAKAMANI,
MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KITUO CHA AFYA CHA MISASI KWA AJILI
YA UCHUNGUZI NA UTAMBUZI, PINDI UCHUNGUZI UKIKALIKA UTAKABIDHIWA
KWA NDUGU WA MAREHEMU KWA MAZISHI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED
MSANGI ANATOA WITO KWA WAENDESHAJI WA VYOMBO VYA MOTO AKIWATAKA
KUZINGATIA ALAMA NA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI, LAKINI PIA
ANAWATAKA WATEMBEA KWA MIGUU KUWA MAKINI WAKATI WOTE PINDI
WANAPOKUWA BARABARANI ILI KUEPUSHA VIFO VINAVYOWEZA KUEPUKIKA.
IMETOLEWA NA,
DCP: AHMED MSANGI
KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA

Das könnte Ihnen auch gefallen