Sie sind auf Seite 1von 3

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI


20 KIVUKONI
FRONT,
P.O. BOX
9000,
11466 DAR ES

Simu: 255-22-2114615, 21190612


Barua pepe: nje@nje.go.tz
Barua pepe: gcu@nje.go.tz
Tovuti : www.foreign.go.tz
Nukushi: 255-22-2116600

SALAAM,
Tanz
ania.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


Taarifa ya ufafanuzi kuhusu Mkutano wa Tume ya Pamoja
ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Malawi
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
ilikutana na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam tarehe 26
Januari, 2017 kwa ajili ya kutoa taarifa kwa umma kuhusu
Mkutano wa Nne wa Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano
(JPCC) kati ya Tanzania na Malawi ambao umepangwa kufanyika
mjini Lilongwe, Malawi tarehe 03 hadi 05 Febuari 2017.
Hata hivyo, vyombo vingi vya habari hususan Magazeti ya tarehe
27 Januari, 2017 vimeandika kwamba Mkutano huo ni maalum
kwa ajili ya kujadili mgogoro wa Mpaka kati ya Tanzania na Malawi
kwenye Ziwa Nyasa pamoja na kesi ya Watanzania nane
waliokamatwa kwa madai ya kuingia nchini Malawi bila kibali.
Wizara inapenda kuchukua nafasi hii kutoa ufafanuzi kwamba,
suala la mgogoro wa mpaka limekwishatolewa taarifa na Wizara
hivi karibuni kwamba lipo chini ya Jopo la Usuluhishi linaloundwa
na Viongozi Wastaafu wa Afrika kutoka nchi za Ukanda wa
Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC). Jopo hilo
linaongozwa na Mhe. Joachim Chissano, Rais Mstaafu wa Msumbiji

akisaidiwa na Mhe. Festus Mogae, Rais Mstaafu wa Botswana na


Mhe. Thabo Mbeki, Rais Mstaafu wa Afrika Kusini.
Aidha, kuhusu suala la Watanzania nane waliokamatwa kwa
madai ya kuingia nchini Malawi bila kibali lipo Mahakamani hivyo
halitakuwa sehemu ya mazungumzo ya Mkutano wa Tume ya
Pamoja.
Pia, Wizara inapenda kuujulisha umma kuwa licha ya kuwepo kwa
mgogoro wa mpaka wa Tanzania na Malawi katika Ziwa Nyasa,
mahusiano ya nchi hizi mbili yamezidi kuimarika siku hadi siku
katika nyanja zote za kiuchumi, kisiasa na kijamii. Hata wananchi
wa pande zote mbili za Ziwa wameendelea kuishi kwa amani na
ushirikiano wa karibu.
Kwa mantiki hiyo, Mkutano wa Nne wa Tume ya Pamoja ya
Ushirikiano kati
Tanzania na Malawi ni njia mojawapo ya
kuendelea kuimarisha mahusiano baina ya nchi hizi mbili.
Mkutano huu ambao ni wa kawaida, una lengo la kujadili na
kutathmini hatua zilizofikiwa katika utekelezwaji wa makubaliano
yaliyofikiwa katika Mkutano wa Tatu wa JPCC uliofanyika Tanzania,
tarehe 24 hadi 30 Juni, 2003.
Aidha, mkutano huu utawaleta pamoja watalaam wa nchi hizi
mbili kutoka Sekta mbalimbali kwa lengo la kujadili changamoto
za ushirikiano katika sekta hizo, kubaini maeneo mapya ya
ushirikiano pamoja na kuweka mikakati ya kutekeleza miradi ya
pamoja itakayokubaliwa baina ya pande hizi mbili. Masuala
mbalimbali ya ushirikiano yatakayojadiliwa kwenye mkutano huu
yatahusu sekta za biashara na uwekezaji, usafirishaji, fedha,
nishati, utalii, ulinzi na usalama uhamiaji, uvuvi na ardhi.
-MwishoImetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,

Dar es Salaam, 27 Januari, 2017

Das könnte Ihnen auch gefallen