Sie sind auf Seite 1von 3

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI


JESHI LA POLISI TANZANIA

TELEGRAMS: POLISI, OFISI YA


TELEPHONE: 2500712 KAMANDA WA POLISI,
Fax: 2502310 MKOA WA MWANZA,
E-mail: mwapol@yahoo.com S.L.P. 120,
rpc.mwanza@tpf.go.tz MWANZA.

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA KWA VYOMBO


VYA HABARI LEO TAREHE 04.06.2017

MTU MMOJA AMEKUTWA AKIWA AMEJINYONGA HADI KUFA KWA KUTUMIA KAMBA
YA MANILA WILAYANI ILEMELA.

MTU MMOJA AMEUAWA NA KUNDI LA WATU WALIOJICHUKULIA SHERIA MKONONI


KWA KOSA LA WIZI WA KUKU WILAYANI MISUNGWI.

WATU WATATU WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA KOSA LA KUPATIKANA NA


MADAWA YA KULEVYA AINA YA BHANGI NA HEROINE WILAYA YA ILEMELA.

KATIKA TUKIO LA KWANZA;

KWAMBA TAREHE 03.06.2017 MAJIRA YA SAA 06:00HRS ASUBUHI KATIKA MTAA WA KITANGIRI
KATA YA KITANGIRI WILAYA YA ILEMELA JIJI NA MKOA WA MWANZA, KULWA MABULA MIAKA 37,
MKAZI WA MTAA WA KITANGIRI AMEKUTWA AKIWA AMEJINYONGA HADI KUFA KWA KUTUMIA
KAMBA YA MANILA ALIYOKUWA AMEIFUNGA KWENYE MTI ULIOKUWA KANDO YA BARABARA YA
KITANGIRI, KITENDO AMBACHO NI KOSA KISHERIA.

INASEMEKANA MAREHEMU ALIKUWA NA MGOGORO WA KIMAPENZI NA MTU ALIYEKUWA NA


MAHUSIANO NAE, KUTOKANA NA MGOGORO HUO KUDUMU KWA MUDA MREFU NDIPO TAREHE
TAJWA HAPO JUU ALIAMUA KUCHUKUA MAAMUZI YA KUJITOA UHAI.

POLISI WAPO KATIKA UCHUNGUZI KUHUSIANA NA MAUAJI HAYO, MWILI WA MAREHEMU


UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA RUFAA YA BUGANDO KWA AJILI YA UCHUNGUZI, PINDI
UCHUNGUZI UKIKAMILIKA UTAKABIDHIWA KWA NDUGU WA MAREHEMU KWA AJILI YA MAZISHI.

KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA KAMISHINA MSAIDIZI WA POLISI ZARAU


MPANGULE ANATOA WITO KWA WAKAZI WA JIJI NA MKOA WA MWANZA AKIWATAKA KUACHA
TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWANI NI KOSA KISHERIA, BALI PINDI
WANAPOKUWA KWENYE MIGOGORO AIDHA YA NDOA AU MAHUSIANO AU YA AINA YOYOTE ILIE
WAWAELEZE WAZEE WENYE BUSARA NA HEKIMA, AU MWENYEKITI WA MTAA AU VYOMBO VYA
DOLA ILI KUWEZA KUEPUSHA VIFO VYA AINA KAMA HII AMBAVYO VINAWEZA KUZUILIKA.

KATIKA TUKIO LA PILI;

MNAMO TAREHE 03.06.2017 MAJIRA YA SAA 10:30HRS ASUBUHI KATIKA KIJIJI CHA MWANANGWA
KATA YA MABUKI WILAYA YA MISUNGWI MKOA WA MWANZA, MTU MMOJA MWANAMUME
AMBAYE BADO HAJAFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI ANAYEKADIRIWA KUWA NA UMRI KATI YA
MIAKA 25 HADI 30, ALIUAWA NA KUNDI LA WATU WALIOJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWA
KUMPIGA MAWE NA FIMBO SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE KISHA BAADAE KUMCHOMA
MOTO KWA KOSA LA WIZI WA KUKU WAWILI, KITENDO AMBACHO NI KOSA LA JINAI.

INADAIWA KUWA MAREHEMU ALIKAMATWA NA WANANCHI AKIWA NA KUKU WAWILI AMBAO


AMEWAIBA KATIKA MOJA YA NYUMBA KIJIJINI HAPO, INASEMEKANA BAADA YA WANANCHI WA
KIJIJINI HAPO KUMKAMATA WALIANZA KUMHOJI HUKU WAKIMPIGA KWA MAWE NA FIMBO
SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE KISHA BAADAE KUMCHOMA MOTO.

WATU/ WASIRI WALITOA TAARIFA POLISI KUHUSIANA NA MAUAJI HAYO AMBAPO ASKARI
WALIFANYA UFUATILIAJI WA HARAKA HADI ENEO LA TUKIO, NA KUFANIKIWA KUWAKAMATA
WATU WATANO WANAODAIWA KUHUSIKA KWA NAMNA MOJA AU NYINGINE KATIKA
KUFANIKISHA MAUAJI HAYO. AIDHA POLISI WAPO KATIKA UPELELEZI NA MAHOJIANO NA
WATUHUMIWA PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA WATAFIKISHWA MAHAKAMANI, MWILI WA
MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA WILAYA YA MISUNGWI KWA AJILI YA UCHUNGUZI NA
UTAMBUZI.

KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA KAMISHINA MSAIDIZI WA POLISI ZARAU


MPANGULE ANATOA WITO KWA WAKAZI WA JIJI NA MKOA WA MWANZA AKIWATAKA KUACHA
TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI PINDI WANAPOWAKAMATA WAHALIFU KWANI NI
KOSA LA JINAI, BALI WATOE TAARIFA POLISI AU WAMFIKISHE MTUHUMIWA KWENYE KITUO CHA
POLISI ILI HATUA STAHIKI ZA KISHERIA ZIWEZE KUCHUKULIWA DHIDI YAKE.

KATIKA TUKIO LA TATU;

KWAMBA TAREHE 03.04.2017 MAJIRA YA SAA 12:00HRS KATIKA MTAA WA SABASABA KATA YA
KISEKE WILAYA YA ILEMELA JIJI NA MKOA WA MWANZA, ASKARI WAKIWA KWENYE DORIA NA
MISAKO WALIFANIKIWA KUWAKAMATA WATU WATATU WAKIWA NA MADAWA YA KULEVYA, KATI
YAO WAWILI AMBAO NI 1.ALLY SALEHE MIAKA 47, MKAZI WA NYASAKA NA 2.WILIAM MAGOMA,
MIAKA 31, MKAZI WA NYASAKA, WALIKAMATWA WAKIWA NA MADAWA YA KULEVYA AINA YA
BHANGI KIASI CHA MISOKOTO 52, HUKU WA TATU ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA PASCHAL
LUSOZI MIAKA 47, MKAZI WA NYASAKA ALIKAMATWA AKIWA NA MADAWA YA KULEVYA
YADHANIWAYO KUWA NI YA HEROINE KIASI CHA PINCHI 10, KITENDO AMBACHO NI KOSA
KISHERIA.

AWALI ASKARI WALIPOKEA TAARIFA KUTOKA KWA WASIRI KWAMBA KATIKA MTAA TAJWA HAPO
JUU WAPO BAADHI YA WATU WANAOJIHUSISHA NA BIASHARA HARAMU YA MADAWA YA
KULEVYA. KUTOKANA NA TAARIFA HIZO ASKARI WALIANZA KUFANYA UPELELEZI NA MISAKO
KATIKA MAENEO HAYO NDIPO TAREHE TAJWA HAPO JUU WATUHUMIWA WATATU WALIWEZA
KUTIWA NGUVUNI HUKU WAKIWA NA AINA HIZO ZA MADAWA YA KULEVYA.

POLISI WAPO KATIKA UPELELEZI NA MAHOJIANO NA WATUHUMIWA WOTE WATATU, PINDI


UCHUNGUZI UKIKAMILIKA WATAFIKISHWA MAHAKAMANI, AIDHA UPELELEZI NA MSAKO WA
KUWATAFUTA WATU WENGINE WANAOJIHUSISHA NA BIASHARA HARAMU ZA MADAWA YA
KULEVYA BADO UNAENDELEA.

KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA KAMISHINA MSAIDIZI WA POLISI ZARAU


MPANGULE ANATOA RAI KWA WAKAZI WA JIJI NA MKOA WA MWANZA HUSUSANI VIJANA
AKIWATAKA KUACHA TABIA YA KUJIHUSISHA AIDHA NA UUZAJI,UTUMIAJI AU USAFIRISHAJI WA
MADAWA YA KULEVYA KWANI NI KOSA LA JINAI, NA ENDAPO MTU ATABAINIKA HATUA STAHIKI
ZA KISHERIA ZITACHUKULIWA DHIDI YAKE. AIDHA PIA ANAWAOMBA WANANCHI WA MKOA WA
MWANZA KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA JESHI LA POLISI KWA KUTOA TAARIFA MAPEMA
ZA WAHALIFU NA UHALIFUJ, ILI WAWEZE KUKAMATWA NA KUFIKISHWA KATIKA VYOMBO VYA
SHERIA.

IMETOLEWA NA;
ACP: ZARAU MPANGULE
KAIMU KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA

Das könnte Ihnen auch gefallen