Sie sind auf Seite 1von 2

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Simu: +255-22-2112035/40 9 Barabaraya Ohio


Nukushi: +255-2122617/2120486 S.L.P. 9223
Baruapepe: ps@moha.go.tz 11483 DAR ES SALAAM

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


Zimekuwepo taarifa za kuingia nchini kwa wahamiaji haramu kupitia mpaka wetu na
Nchi ya Kenya. Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kupitia Idara yake ya Uhamiaji
inawahakikishia Watanzania kwamba hatua kali za kisheria zinachukuliwa dhidi ya
raia wote wa kigeni wanaoingia nchini kinyume cha Sheria za Uhamiaji na nchi yetu.

Kimsingi hakuna raia yeyote wa kigeni anayeruhusiwa kuingia nchini kwa kisingizio cha
kuja kufanya kazi, biashara au Uwekezaji bila kufuata Sheria na taratibu za Uhamiaji,
na kwamba wote wanaokiuka Sheria hizo watarudishwa makwao mara moja.

Ni jambo lisilokubalika mtu atoke nchini kwake bila kibali cha kufanya kazi Tanzania kwa
madai kwamba alishatuma maombi ya kibali husika na amekuja kusubiri majibu ya
kibali hicho akiwa Tanzania. Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi haitavumilia ukiukwaji
huu wa sheria za nchi na kwamba kila raia wa kigeni anayekusudia kuingia nchini
ahakikishe ana kibali cha kuingia nchini na anafanya kazi ambayo ndiyo aliyoiombea
kwenye kibali chake.

Yapo matukio ya raia wa nchi jirani, hususan katika mipaka ya Kenya na Uganda
ambapo kutokana na hali ya muingiliano wa kiuchumi na kijamii, raia wa nchi zetu,
wamekuwa wakivuka mipaka pande zote kufuata huduma mbalimbali, Hii pia
inachangiwa na mapungufu katika usimamizi wa alama na maeneo ya wazi ya mipaka
yetu. Hali hii inapelekea baadhi ya wananchi wetu kutumia mwanya huo
kuwatengenezea raia wa kigeni mazingira ya kuingia nchini bila kufuata taratibu au
hata kutumiwa katika biashara haramu ya kusafirisha binadamu.

Tahadhari inatolewa kwa Watanzania wote ambao wamekuwa wakiwapokea raia hao
wa kigeni na kuwahifadhi, kwani kufanya hivyo ni kuvunja sheria za nchi ikiwemo ile
Sheria ya usafirishaji haramu wa binadamu.

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kupitia Idara yake ya Uhamiaji imeanza kuchukua
hatua ili kuweza kushughulikia suala hili. Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dk. Anna
Makakala, tayari ametembelea baadhi ya maeneo ya mipaka yetu hususani kijiji cha
Jasini wilayani Mkinga mkoani Tanga ili kujionea hali halisi na kutoa Maelekezo ya
hatua za kuchukua kudhibiti hali hiyo kwa mujibu wa Sheria, kwa kuwa eneo hilo
linaonyesha kuwa na muingilino baina ya nchi ya Kenya na Tanzania kwa muda mrefu.

Wizara itaendelea na Mashauriano na Mamlaka nyingine zenye dhamana ya


Kusimamia alama za mipaka ya nchi yetu kwa kuwa tatizo hili la muingiliano wa
wananchi wa pande zote lipo kwenye mipaka mingi ya nchi.

Imetolewa na
Christina R. Mwangosi
Kaimu Msemaji
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
4 Agosti 2017

Das könnte Ihnen auch gefallen