Sie sind auf Seite 1von 2

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA


ISO 9001:2015 CERTIFIED

TAARIFA KWA UMMA

MAWAKALA WANAOSAJILI LAINI ZA SIMU BILA IDHINI

Wakati Mamlaka ya Mawasiliano Tanzaia (TCRA) inaendela na utekelezaji wa zoezi la


usajili wa laini za simu kwa njia ya biometria, TCRA imebaini kuwa kuna watu
wanaojihusisha na usajili wa SIMU bila kuidhinishwa na watoa huduma za mawasiliano.

Kwa mujibu wa kifungu cha 92 na 97 cha Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na


Posta, 2010 na Kanuni ya 9,10, na 11 ya Kanuni za Usajili wa Laini za Simu (Sim Card
Registration Regulations, 2018), TCRA inapenda kuutaarifu na kuukumbusha Umma
kuwa:-

1. Ni marufuku kwa mtu yeyote kuuza, kusambaza au kusajili laini za simu bila
kuwa na uthibitisho kuwa ameidhinishwa na mtoa huduma za mawasiliano kutoa
huduma hizo;

2. Yeyote anayejihususha na uuzaji, usambazaji au usajili wa laini za simu


anatakiwa kuwa na ofisi ya kutolea huduma hiyo ya usajili wa laini za simu; na

3. Ni kosa la jinai kwa mtu yeyoye kuuza, kusambaza au kusajili laini za simu bila
kuwa na ofisi na uthibitisho wa idhini ya mtoa huduma husika.

Umma unakumbushwa na kuonywa kuwa hatua zaidi zitachukuliwa, ikiwa ni pamoja na


kufikishwa mahakamani pamoja na faini, kwa mtu yeyote atakaye bainika kuuza,
kusambaza au kusajili laini za simu bila kufuata taratibu.

Imetolewa na:

Mkurugenzi Mkuu,
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania,
Jengo la Mawasiliano,
Kitalu Na. 20 Barabara ya Sam Nujoma,
S. L. P 474,
14414 DAR ES SALAAM
THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
TANZANIA COMMUNICATIONS REGULATORY AUTHORITY
ISO 9001:2015 CERTIFIED

PUBLIC NOTICE
UN-AUTHORISED SIM CARDS REGISTRATION AGENTS/DEALERS
While the Tanzania Communications Regulatory Authority (TCRA) commends the
general public on the positive response regarding the ongoing SIM card registration
exercise, it has come to the attention of the Authority that there are persons involved
with SIM registration without authorization from relevant mobile network operators.

In accordance to Sections 92,97 of EPOCA and Regulations 9,10, and 11 of the


Electronic and Postal Communications (Sim Card Registration) Regulations, 2018, TCRA
would like to inform and remind the general public that:-

1. Any person is not allowed to sell, distribute or register a detachable SIM card or
built-in SIM card mobile telephone without evidence of prior authorization of the
respective mobile service provider;

2. Any person who sells, distributes or registers SIM Cards must have an office with
physical location for the registration; and

3. Any person who sells, distributes or registers detachable SIM card or built-in SIM
card mobile telephone without an office with physical location and prior
authorization of respective application service licensee commits an offence.

Take notice and be warned that further action, including prosecution and imposition of
fines, will be taken against any person found to be selling or distributing SIM cards
without prior authorization of the respective mobile service provider.

Issued by:

Director General,
Tanzania Communications Regulatory Authority,
Mawasiliano Towers,
Plot 20 Sam Nujoma Road,
P. O. Box 474,
14414 DAR ES SALAAM

Das könnte Ihnen auch gefallen